TIMU za wanawake za Ilala na Kinondoni zimefuzu fainali
ya mashindano ya Airtel Rising Stars zinazochezwa Uwanja wa Karume jijini Dar
es Salaam.
Ikicheza kwa ustadi mkubwa timu ya Kinondoni iliweza
kuibugiza bila huruma timu ya mkoa wa Kigoma kwa mabao 7-0 katika mechi ya
asubuhi.
Mabao ya ushindi yaliwekwa kimiani na wachezaji Sherida
Boniface aliyefunga mabao manne katika dakika za 10, 14, 6, 38 na mabao mengine
yalifungwa na Tatu Iddi dakika ya 7, Shamimu Khamisi dakika 23 na Christina
Daudi dakika ya 40.
Katika mechi ya pili iliyo wakutanisha timu za Ilala
na Temeke, Ilala ilifanikiwa kutinga fainali baada ya kuichapa Temeke kwa
mikwaju ya penati 2-0 baada ya kutoshana nguvu ya bao 1-1 katika muda wa
kawaida.
Mabao katika muda wa kawaida kwa timu ya Temeke lilifungwa
na Donisia Daniel dakika 32 na Neema Paul wa Ilala alisawazisha bao hilo dakika
50 na kufanya matokeo kuwa 1-1 hadi dakika 90
No comments:
Post a Comment