Hii ndiyo kambi mpya ya Coastal Union ya Tanga ambayo iko katika eneo la ufukwe, Raskazone mjini Tanga.
Kambi hii ndiyo ya kisasa zaidi kuliko nyingine zinazotumiwa na timu za Ligi Kuu Bara kutokana na marekebisho makubwa iliyofanyiwa.
Wachezaji wake watakuwa wakiishi hapo, ikiwa ni pamoja na sehemu maalum kwa ajili ya kucheza pool na michezo mingine kama playstation.
Kila chumba kitakuwa na kiyoyozi ili kuwafanya wachezaji hao kuishi katika mazingira bora zaidi.
Mkurugenzi wa Ufundi wa Coastal, Mohammed Bin Slum amesema wameamua kufanya hivyo kwa lengo la kuhakikisha wachezaji wao wanaishi vizuri, kula vizuri na kujiandaa vizuri.
Walimu na watu wengine wa benchi la ufundi watakuwa wakiishi katika eneo hilo.
Coastal Union tayari imeanza mazoezi mjini Tanga kujiandaa na msimu mpya wa 2013-14 huku wachezaji wake Haruna Moshi ‘Boban’ na Juma Nyosso wakiwa wameungana na wenzao.
No comments:
Post a Comment