Gonzalo Higuain (kushoto) alikuwa karibu ajiunge na Arsenal lakini huenda Napoli ikapiku jitihada zao.Leandro Damiao akigombea mpira wakati wa michuano ya Confederations Cup
Rais wa Napoli Aurelio De Laurentiis amedai kuwa klabu yake ina kiasi cha pauni milioni £108 katika mpango wake na iko katika mazungomzo ya kuwasajili Gonzalo Higuain na Leandro Damiao.
Arsenal kwasasa ipo katika mawingo ya kumnasa nyota wa Real Madrid Higuain wakati ambapo Totenham wakiwa katika mpango wa kumchukua Damiao wa Internacional lakini inavyoonekana ni kwamba Rafa Benitez huenda akazidi mawindo ya vilabu hivyo na kufanikiwa kuwachukua nyota hao na kuwapelekea Italia.
Napoli inahitaji mshambuliaji baada ya kumuuza Edinson Cavani aliyejiunga na PSG na wanajeuri ya pesa ya kufanya hivyo ikiwa nji pamoja na pauni milioni £55 za Cavani.
Kupitia mtandao wa wa kijamii wa Twitter alikuwa akichati na mashabiki Rais huyo wa Napoli Aurelio De Laurentiis amesema ni kweli wanawanata Higuain na Damiao.
'Raul Albiol mlinzi wa Madrid anaendelea na vipimo vya afya na tunamatumaini atafanikiwa' .
Napoli tayari imeshakubali kumsajili mshambuliaji wa Hispania Jose Callejon kutoka kawtika klabu ya Real Madrid na kumchukua winga wa kimataifa wa Belgium Dries Mertens.
No comments:
Post a Comment