Kocha Mkuu wa Uganda Cranes, Milutin Sedrojevic ameongeza wachezaji tisa katika kujiimarisha na mchezo wa marudiano dhidi ya Taifa Stars utakaochezwa Julai 27, mwaka huu utakaochezwa Uwanja wa Namboole mjini Kampala
Micho amesema kuwa mchezo huo wa marudiano na Tanzania ni muhimu kwani umebaki kulinda heshima na
kusafisha njia ya kufuzu klabu bingwa Afrika kwa wachezaji wa ndani.
"Ushindi wetu dhidi ya Tanzania jijini Dar es salaam umenipa
ujasiri kuelekea hatua ya kufuzu, lakini
kazi ni mbali na kumaliza", alisema kocha huyo mzaliwa wa Serbia.
Uganda the cranes waliifunga Taifa stars bao 1-0 lilifungwa na Dennis Iguma dakika ya 48 na timu
hiyo imeanza mazoezi leo Jumatano asubuhi.
Micho amemwita Augustine Nsumba, ambaye mara ya mwisho
kuchezea Cranes ni mwaka 2006, kipa kijana, Ismail Watenga, beki wa katikati,
Hashim Ssempala na Willy Kavuma, na watatu toka kwa timu za U-23 ni winga wa kushoto,
Azizi Kémba na washambuliaji, Daudi
Kasirye na Simon Okwi.
Wengine walioitwa kufanya mauaji dhidi ya Taifa stars ni Augustine Nsumba, Willy Kavumu, William Wadri and
Habibu Kavuma
Uganda itawakosa Mshambuliaji, Patrick Mapafu, ambaye
amekwenda nchini Ureno kufanya majaribio na Striker, Tonny Odur, ambaye alikuwa
kikosi cha kwanza na Mapafu dhidi ya Tanzania ambaye alipata majeraha sasa
nafasi yake itachukuliwa na ama Simon Okwi
au Daudi Kasirye.
Uganda itacheza mchezo wa kirafiki Ijumaa kabla ya kuingia na kambini Jumatatu
ijayo.
Timu Kamili iliyoitwa ni
Makipa ni : Muwonge Hamza (nyoka), Kimera Ali (SC VU) na
Ismail Watenga (nyoka)
Mabeki: Wadada Nicholas (Sc nyoka), Iguma Denis (Sc Vu),
Kasaaga Richard (Kiira Young Fc), Hashim Ssempala (Bul-Bidco), Yusuf Mukisa
(Proline), Kawooya Fahad (KCC Fc), Kisalita Ayub (Villa) na Savio Kabugo (SC
VU).
Mid fielders: Ntege Ivan (KCC), Majwega Brian (KCC FC),
Kapteni Hassan Wasswa Mawanda (KCC FC), Mpande Joseph (nyoka), Muganga Ronald
(Sc Villa), Kyeyune Said (URA), Azizi Kémba (Bul- Bidco), Augustine Nsumba
(URA) na Willy Kavuma (Express).
Washambuliaji: William Wadri (Sc Vu), Simon Okwi (KCC),
Daudi Kasirye (URA) na Frank Kalanda (URA).
No comments:
Post a Comment