LONDON, England
MCHEZAJI,
Mikel Arteta amempa somo kocha wa Arsenal, Arsene Wenger akimueleza kuwa ni wakati muafaka
kwa timu hiyo kujiunga kwenye msafara wa timu zinazotumia fedha nyingi.
Tayari kocha huyo wa Arsenal, ameshatangaza kuachana na maisha ya
ubahili aliokuwa nao kwa muda mrefu, akisema kuwa atafanya makubwa wakati wa
usajili wa majira haya ya joto.
Kutokana na ahadi hiyo na Arteta
hakusubiri kumpasha akisema kuwa ataupokea kwa mikono miwili usajili wa
wachezaji nyota kutokana na kwamba,
anaamini kipindi hiki ni cha kupigania ubingwa.
Mhispania huyo kwa sasa anaonekana
kubadili mawazo, baada ya miaka miwili ya hofu kuwa atakuwa nyota mwingine
atakayeondoka.
“Klabu imeshatangaza wazi kuwa tunataka kuwa
tishio na mimi nalipongeza hilo.
“Baadhi ya wachezaji tunaohusishwa nao wananifanya nijisikie mwenye
furaha,” aliongeza.
Kwa sasa Gunners inadaiwa kujiandaa
kutumia pauni milioni 35, kwa ajili ya kumnasa nyota wa Liverpool, Luis Suarez huku ikihusishwa kuwa kwenye harakati za
kuwanasa, Gonzalo Higuain na Wayne Rooney.
No comments:
Post a Comment