Suarez akitembea katika njia ya kutokea uwanjani kuelekea katika mchezo baina ya Liverpool na Melbourne mchezo ambao Liverpool walichomoza na ushindi wa mabao 2-0.
Suarez akishuka uwanjani kwa mara ya kwanza na kuvalia jezi ya Liverpool tangu kwa mara ya mwisho kufanya hivyo April 21.
Suarez alianzia benchi kabla ya kuingia kunako dakika ya 70.
Brendan Rodgers anaamini kuwa kurejea kwa Luis Suarez itaakuwa ni dhihirisho la kushinda vita ya kumbakisha mshambuliaji huyo katika katika klabu yake ya Liverpool.
Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Uruguay ambaye amekuwa katika mvutano mkubwa wa tetesi za kutaka kuelekea kwa washika bunduki la London Arsenal, hii leo alikuwa katika wingu kubwa la kelele za mashabikiwa 95,446 waliofurika uwanjani hususani wakati akiingia kunako dakika ya 72 katika mchezo ambao Liverpool iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Melbourne Victory huko MCG.
Suarez ndiye aliyetengeneza bao la pili la Liverpool baada ya kugeuka na kuachia mpira wa krosi ulimkuta Iago Aspas baada ya kupata mpira wa kona fupi kutoka kwa Stewart Downing.
Steven Gerrard ndiye aliyefunga bao la kwanza baada ya jitahada zake binafsi.
Arsenal iliwashitua Liverpool hapo jana kwa kutangaza ofa nono ya pauni milioni £40,000,001 kujaribu kuvunja mkataba wa Suarez lakini Rodgers anasisitiza kuwa hakuna kitakacho badilisha msimamo wa klabu yake juu ya mshambuliaji huyo na kusema anataka mshambuliaji huyo kusalia Anfield.Suarez bado anapendwa na mashabiki wa Liverpool na amepata mapokezi mazuri na kulakiwa na mashabiki hao baada ya mchezo wa leo.
Suarez akisani autograph baada ya mchezo huko Melbourne Cricket Ground.
Huu ulikuwa ni umati mkubwa kuwahi kushuhudiwa liverpool ikicheza mbele ya mashabiki wa 100,000 yangu kutokea hivyo katika fainali ya FA mwaka 1986 walipocheza dhidi ya Everton na Rodgers amekiri kupata mapokezi makubwa yeye wachezaji wake na maafisa wengine wa timu hiyo tangu kuwepo kwake Australia.
No comments:
Post a Comment