Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, July 4, 2013

JKT YAANZA MASHINDANO YA KUSHEREHEKEA MIAKA 50 YA JESHI HILO

Mkuu wa JKT Meja Jenerali Raphael Muhunga akitoa hotuba yake wakati wa uzinduzi wa michezo ya kusherehekea miaka 50 ya JKT iliyoanza leo katika viwanja vya Kumbukumbu ya Karume jijini Dar es Salaam. (Picha na Habari Mseto Blog) Baadhi ya wachezaji wakipita kwa maandamano mbele ya mgeni rasmi wakati wa uzinduzi wa michezo ya kusherehekea miaka 50 ya JKT. Macho mbeleee. Mkuu wa JKT Meja Jenerali Raphael Muhunga akisalimiana na wachezaji wa timu ya Kanembwa JKT ya Kigoma.
Mkuu wa JKT Meja Jenerali Raphael Muhunga akisalimiana na wachezaji wa JKT Ruvu kabla ya mpambano wao na Kanembwa JKT. Mgeni rasmi akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu zote mbili.


MKUU wa Jeshi la Kujenga Taifa, Meja Jenerali Rafael M. Muhuga, amesema JKT inajivunia kuibua vipaji vya michezo mbalimbali na kuendeleza pia kuwa na timu zenye ushindani mkubwa kwenye soka la Tanzania.

Muhuga aliyasema hayo jana wakati akifungua mashindano ya kuadhimisha miaka 50 ya Jeshi la Kujenga Taifa kwenye Uwanja wa Karume uliopo Ilala jijini Dar es Salaam nakuwataka wachezaji wanaoshiriki mashindano wacheze  kwa kufuata taratibu kuepuka kuumiza.

Pia alisema kauli mbiu ya mashindano hayo ni  ‘Tunajivunia malezi bora ya vijana, uzalishaji mali, Ulinzi na linasonga mbele’ na ndio maana serikali imeamua kurudisha JKT kwa vijana ili wapate malezi borana kuzalisha mali huku wakiendekleza pia ulinzi wa nchi.

Mashindano hayo yanashirikisha michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu, mpira wa kikapu, mpira wa pete, wavu, mpira wa mikono,  ngoma na michezo mingine yote.

Kwenye mchezo wa ufunguzi timu ya JKT Ruvu inayoshiriki ligi kuu ya Tanzania bara ilishindwa kutamba mbele ya JKT Kanembwa inayoshiriki ligi daraja la kwanza Tanzania bara baada ya kumaliza dakika 90  bila kufungana.

Hata hivyo washambuliaji wa JKT Ruvu  wakiongozwa na Musa Mgosi  walikosa mabao ya wazi mara kadhaa kwenye kipindi cha kwanza huku beki wao Stanley Nkomola akifanya kazi ya ziada kumkaba Mfaume Peter kiungo mshambualiaji wa JKT Kanembwa kutokana na kuliandama lango lao.

Mchezo mwingine ulizikutanisha JKT Oljoro na Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Bandari, Kurasini ambapo JKT Oljoro ilishinda kwa bao 1-0.

Timu za soka zinazoshiriki mashindano hayo ni JKT Oljoro, JKT Mgambo, JKT Ruvu, Ruvu Shooting, JKU ya Zanzibar, JKT Mlale na JKT Kanembwa.

No comments:

Post a Comment