Ally Hassan Mwinyi unavyoonekana kwa nje |
VIWANJA sita vya soka vipo hatari kufungiwa na kamati ya
ligi Kuu ya Tanzania Bara endapo wamiliki hawatavifanyia marekebisho.
Akizungumza jijini, akiwa ofisini kwake, Mkurugenzi wa
Ligi hiyo Silas Mwakibinga alisema viwanja ambavyo vinaweza kufungiwa ni Ally
Hassan Mwinyi -Tabora, Sheikh Abeid –Arusha, Kaitaba-Kagera, Sokoine – Mbeya,
Jamhuri – Morogoro na Mkwakwani – Tanga.
“Hatutaona aibu kufungia viwanja ambavyo vitakuwa havikidhi
kuchezewa Ligi Kuu kwa msimu wa 2013/14 hivyo wahusika wanatakiwa wahakikishe
viwanja vinafanyiwa marekesho kama nilivyowajulisha kwenye barua”, alisema
Mwakibinga
Pia alisema kiwanja
kina sababu inayofanya kufungiwa ikiwa ni pamoja na kukosa vyoo, maji,
sehemu ya kuchezea kutokuwa nzuri na uzio wa kuzuia sehemu ya kuchezea na
mashabiki.
Mwakibinga alitolea mfano uwanja wa Sheikh Abeid na Sokoine
kuwa sehemu ya kuchezea nyasi zake ni mbaya kwani zinaota kwa kujenga matuta
madogo madogo ambayo yanasababisha kupoteza uwelekeo wa mpira pindi unapodunda.
Uwanja wa Ally Hassan Mwinyi wa Tabora wenyewe hauna uzio wa
kutenganisha sehemu ya kuchezea na sehemu wanazokaa mashabiki jambo ambalo
kisheria halitakiwa hivyo unakosa sifa za kuchezewa Ligi Kuu.
Amewataka viongozi wa vyama vya soka kushirikiana na
wamiliki wa viwanja hivyo ili kuvifanyia marekebisho kabla ukaguzi haujaanza
kwani ukaguzi ukifika na kukuta bado havijarekebishwa watavifungia.
Kaitaba |
No comments:
Post a Comment