Marafiki: Pique na Fabregas wamekuwepo Hispania na katika klabu ya Barcelona pamoja. Gerard Pique amewaonya Manchester United juu ya harakati zao za kumtaka kiungo Cesc Fabregas akisema kuwa wanapotez muda wao katika kujaribu kung'oa Barcelona. David Moyes jana alithibitisha juu ya dhamira ya United kwa mara ya pili kumtaka kiungo huyo angalau kwa kuongeza dau na kufikia pauni za milioni £30 na ziada ya mambo mengine huku klabu hiyo kutoka Katalan ikitupilia mbali ofa hiyo kwa mara ya pili lakini maafisa wa Old Trafford wakionekana kung'ang'ania tena kwa mpango mwingine wa kuongeza dau lingine na kufikia pauni milioni £35 siku za usoni. Wakati hayo yakiendelea, mlinzi wa kati na nahodha wa Barcelona Gerard Pique, ambaye aliichezea United wakati huo chini ya Sir Alex Ferguson kwa miaka minne kati ya 2004 na 2008, ameweka wazi kuwa Fabregas hana nia ya kuondoka Camp Nou na kurejea katika ligi kuu ya England Barclays Premier League na kuitumikia United.
Pique amenukuliwa na gazeti la The Sun akisema ‘United inapoteza muda. Ilimchukua muda mrefu kwa Cesc kufikiria kurejea nyumbani na hatakata tamaa. Hapa ni nyumbani. Ni sehemu ilipo familia take, na anacheza akiwa karibu na marafiki zake. Ametuambia anafuraha na amedhamiria kusalia na Barcelona.’
Moyes anakabiliwa na jaribio gumu akisaka saini ya mchezaji mkubwa, ilhali Barcelona ikiweka ngumu mpango wao huo kwa kiungo huyo wa Hispania wakati ambapo Josep Maria Bartomeu, ambaye makamu wa Rais wa klabu hiyo wiki iliyopita akikazia kauli yake kuwa Fabregas hayuko sokoni.David Moyes amesema kuwa United imefanya tena mpango mwingine kwa ajili ya Fabregas.
Kama hiyo haitoshi United imeendelea kuwa na matumaini ya kufikia katika kilele cha mpango wao huku makamu mwenyekiti Ed Woodward akiongoza majadiliano licha ya kwamba Moyes muda utafika kwa United kukata tamaa katika ushawishi wao na kufikiria mawingo mengine.
No comments:
Post a Comment