Ocean Mushure alifunga penato ya ushindi kwa washindi hao mara nne wa michuano hiyo.Katika muda wa kawaida Zimbabwe walikuwa wa kwanza kushambulia na kuandika bao la uongozi kwa mpira wa kurudi uliofungwa na Masimba Mambare kunako dakika ya.Mshambuliaji wa Malawi James Sangala alitolewa nje yaw a uwanja baada ya kupewa kadi ya pili ya njano kabla ya mapumziko kitendap ambacho kiliivuruga the Flames.
Lakini hata hivyo kunako dakika ya 85 ya mchezo , Boniface Kaulesi alifanikiwa kuandika bao la kuswazisha na mchezo kuelekea katika dakika za nyongeza na hatimaye kufikia katika hatua ya mikwaju ya penati. Katika hatua nyingine Afrika ya kusini nao wamefanikiwa kutinga katika hatua hiyo ya nusu fainali baada ya kuwachapa Namibia kwa bao 2-1 mchezo ambao pia umepigwa hii leo.Bafana Bafana walikuwa wakicheza mechi yao kwanza ya michuano hiyo kufuatia kupata nafasi ya kuingia moja kwa moja katika hayua hiyo
Mchezaji alieingia kutoka benchi Shongwe Jabulani aliandika bao kwanza kwa mpira mrefu muda mfupi baada ya kuanza kipindi cha pili.Afrika kusini pia wakafanikiwa kuandika bao la pili kupitia kwa Kekana Hlompho akiwa katika kona ya kisanduku cha hatari.
Namibia walifanikiwa kupata penati kufuatia Mkhwanazi Buhlke kuunawa mpira ndani ya kisanduku cha 18 lakini hata hivyoWilly Stephanus alishindwa kuandika bao kwa pigo la kwanza kabla ya mwamuzi kumtaka kurudia penati yake ambapo kiungo huyo aliiukwamisha mpira kambani.
No comments:
Post a Comment