Viongozi wa Simba wakiwa wameshikana mikono kudhihirisha umoja kurejea klabuni
MSHIKAMO umerejea kwenye klabu ya
Simba kufuatia Mkutano uliofanyika leo baina ya uongozi wa klabu
na viongozi wa matawi yote ya Simba jijini Dar es Salaam katika makao makuu ya
klabu.
Mkutano huo uliitishwa baada ya Makamu Mwenyekiti wa Simba, Geofrey Nyange na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Zacharia Hans Poppe, kujiuzulu nyadhifa zao ndani ya klabu hivi karibuni.
Mkutano huo ulikuwa chini ya Kaimu Makamu Mwenyekiti wa Simba, Joseph Itang'are, na Malkia wa nyuki na kuhudhuriwa na Wenyeviti na Makatibu wa Matawi yote ya klabu jijini Dar es Salaam.
Itang'are, maarufu kwa jina la Mzee
Kinesi, aliueleza mkutano huo mwenendo wa timu katika mashindano tofauti ambayo
timu inashiriki pia hatua zilizochukuliwa kunusuru hali ya sasa.
"Naomba wanachama wote wa Simba kuendeleza utulivu na mshikamano ndani ya klabu ili tuwe kitu kimoja. Tukiwa kitu kimoja tutaweza kutatua matatizo yetu kwa ufanisi lakini tukigawanyika tutazidi kuharibikiwa," alisema.
"Naomba wanachama wote wa Simba kuendeleza utulivu na mshikamano ndani ya klabu ili tuwe kitu kimoja. Tukiwa kitu kimoja tutaweza kutatua matatizo yetu kwa ufanisi lakini tukigawanyika tutazidi kuharibikiwa," alisema.
Katika mkutano huo, viongozi wa matawi waliahidi kutoa ushirikiano wa kutosha kwa uongozi ili kuhakikisha Simba inashinda mechi zake zote zilizosalia katika Ligi Kuu ya Tanzania ili iweze kuwa miongoni mwa nafasi za juu katika michuano hiyo.
Viongozi hao pia waliunda kwa jopo la watu watano wanaoheshimika ndani ya klabu kwa lengo la kwenda kumshawishi Poppe abadili maamuzi yake. Jopo hilo limetakiwa kuanza kazi mara moja ingawa majina ya wanaounda jopo hilo yatafahamika baadaye.
Katika kuhimiza mshikamano ndani ya klabu, juzi jioni Mwenyekiti wa Kamati ya Ushindi Simba, Rahma Al Kharusi, akifuatana na wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya Simba, walikwenda kwenye Ofisi za Kundi la Mpira Pesa Magomeni Mikumi jijini Dar es Salaam kuanza mchakato wa upatanishi.
Kundi hilo kwa sasa limerudishwa na tofauti zilizokuwepo kati yao na uongozi zilimalizika kwa Malkia wa Nyuki alisema kamati yake haiwezi kufanya kazi vizuri iwapo kuna migogoro ya ndani kwa ndani baina ya wanachama.
"Lengo hapa ni kutafuta suluhu kwa faida ya Simba. Tukigombana wenyewe kwa wenyewe wanaofaidi ni maadui zetu. Tukae chini, tuzungumze na mwisho wa siku tufikie makubaliano kwa faida ya klabu yetu," alisema Al Kharusi.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Mpira Pesa, Ustaadh Masoud, alisema wao hawana nia mbaya dhidi ya Simba isipokuwa kuna mambo ambayo ni lazima yawekwe sawa kwa lengo la kuondoa tofauti zote zilizokuwapo huko nyuma.
Simba kesho inacheza mechi ya Ligi Kuu ya Tanzania dhidi ya Coastal Union kutoka Tanga na matawi yote yameahidi kushiriki kufanikisha ushindi katika mechi hiyo.
No comments:
Post a Comment