Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, February 27, 2013

NADHIPA WA ISIDINGO AITAMANI BONGO MOVIE

MSANII wa Tamthilia ya Isidingo, Hlubi Mboya, Maarufu kama Nantipa, kutoka afrika kusini amekiri kuwa moja ya ndoto zake ni kufanya kazi na wasanii wa filamu wa hapa nchini.


Msanii huyo ambaye ni balozi wa shirika la Chakula duniani WFP, anatarajiwa kuongoza timu ya Wanawake 12 kutoka katika nchi za Tanzania, Nepal na Australia kupanda mlima Kilimanjaro kesho kupitia Geti la Machame lililok wilaya ya Hai, Mkoani hapa.

Alisema wasanii wengi baada ya kupata umaarufu hujisahau na kujikuta wakijiingiza katika matumizi mabaya ya madawa ya kulevya pamoja na kufanya vitendo viovu vinavyomchukiza mungu na kuwataka kuwa na hofu ya Mungu ndani yao.

“Wasanii wengi wanajisahau, swala la kutumia mdawa ya kulevya ni swala la kimaadili, wengi wetu tunakosa uchaji mungu ndani yetu na ndio maana tunapopata umaarufu na fedha nyingi hujikuta tukiingia katika vitendo viovu,” alisema Nantipa.

Msanii huyo anatarajia kuanza kupanda mlima Kilimajaro kesho asubuhi kutokana na safari hiyo kusitishwa hii leo baada ya mizigo yao kupotea hivyo kulazimisha Uongozi wa Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro kuagiza mizigo mingine.

Nantipa katika safari hiyo ataongozana na wanawake wenzake kutoka Nepal, Tanzania na Australia kwa lengo la kuhamasisha usawa wa kijinsia, safari iliyodhaminiwa na shirika la Chakula Duniani (WFP), Cildreach na Really Wild kwa kushirikiana na hifadhi ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA).


KUTOKA KUSHOTO NI MWAKILISHI NA MRATIBU WA WFP NCHINI TANZANIA RICHARD RAGAN, MKUU WA WILAYA YA MOSHI DK.IBRAHIM MSENGI, NA NADIPHA
Akizungumza na Mwanahabari wetu leo asubuhi, Nantipa ambaye aliwahi kuyjizolea umaarufu katika Tamthilia hiyo inayorushwa kila siku na chombo Fulani cha Televisheni hapa nchini, alisema ukiachilia mbali ndoto za kupanda mlima Kilimanjaro mara nyingi amekuwa akitamani kufanya kazi na wasanii wengine wakongwe barani afrika na moja ya nchi anazozihusudu ni Tanzania.

DC MOSHI AKIZUNGUMZA JAMBO NA NADIPHA
“Fursa ya kupanda Mlima Kilimanjaro ni moja ya ndoto zangu kama msanii ndoto ambayo hatimaye kesho (leo) nitaitimiza lakini natamani sana kuwa msanii mkubwa, natamani kufanya kazi na wasanii wakubwa afrika, lakini hasa nafikiria kufanya kazi na msanii wa Tanzania na kujifunza Kiswahili,” alisema Nantipa.

Aidha Msanii huyo mcheshi na mchangamfu alikemea tabia ya wasanii kujiingiza katika matumizi ya madawa ya kulevya na kuongeza kuwa inapasa wasanii wajitambua na kutambua dhima iliyoko mbele yao ya kufundisha jamii na sio kupotoka.
NADIPHA HAKUJIZUIA KUONYESHA FURAHA YAKE
NADIPHA ALIONYESHA KUSHIRIKIANA NA WAANDISHI HABARI MKOA WA KILIMANJARO KUTOKA KUSHOTO SAMUEL SHAO, TADEI MASAWE
NADIPHA NA KHADIJA HAMAD
NADIPHA NA FADHILI ATHUMAN WA BLOGU YA TAIFA LETU

No comments:

Post a Comment