Thursday, February 28, 2013
HARUNA MOSHI "BOBAN" KUIKOSA LIBOLO
Wakati Simba inaondoka kesho alfajiri kwenda Angola kumaliza kibarua chao ambacho walikianza nyumbani dhidi ya FC Libolo , kiungo Haruna Moshi 'Boban' wa Simba hatakuwamo katika kikosi cha timu yake kitakachosafiri kutokana na majeraha.
Boban aliondolewa tangu juzi katika kikosi chao kitakachoondoka kesho alfajiri kwenda kujiandaa kwa mechi hiyo watakayojaribu kubadili matokeo na kusonga mbele baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0 kwenye Uwanja wa Taifa wiki iliyopita.
Daktari wa Simba, Cosmas Kapinga, amesema kuwa Boban hajafanya mazoezi na wenzake tangu walipomaliza mechi ya ligi ya Bara dhidi ya Mtibwa Sugar ambapo walilala bao 1-0. Daktari huyo aliongeza kuwa kutokana na kutokuwa 'fiti', Boban na mshambuliaji wao yosso, Edward Christopher wameondolewa na kocha wao Mfaransa Patrick Liewig katika mipango yake kwa ajili ya maandalizi dhidi ya Libolo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment