Mshambuliaji wa Simba Felix Sunzu hii leo
anatarajiwa kuwepo katika orodha ya wachezaji watakao itumikia timu hiyo katika
mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar mchezo utakao pigwa uwanja wa Taifa
jijini Dar es Salaam Baada ya kuwa nje kwa kipindi kirefu
akijiweka fiti.
Nafasi ya Sunzu kuwepo kikosini hii leo inakuja
kufuatia mshambuliaji huyo raia wa Zambia kufanya vizuri katika mchezo wa
kirafiki kati ya Simba na Mbeya City uliofanyika mkoani Mbeya.
Msemaji wa klabu ya Simba Ezekiel Kamwaga amesema
kiwango kilicho onyeshwa na Sunzu katika mchezo huo ambao mwalimu Patrick Liewig
aliwatumia wachezaji wengi wa kikosi cha pili Sunzu alionyesha kiwango ambacho
kimempa matumaini makubwa mwalimu huyo ya kuanza kumuamini na kumpa nafasi ya
kucheza.
Kiwango cha Sunzu katika siku za hivi karibuni
mimeporomoka sana kutokana na kukabiliwa na maradhi ambayo yamemfanya kupigania
afya yake kwa kipindi kirefu na sasa anaonekana kuwa ameaanza kuwa
fiti.
Wakati hayo yakiwa hivyo, naye mlinzi tegemeo wa
kati wa Simba Shomari Kapombe licha ya kuelezwa kuwa hali yake imeanza kuimarika
kufuatia kupata matibabu ya kuondoa damu iliyovilia katika mishipa yake ya
damu.
Hata hivyo mlinzi huyo wa hatakuwepo katika kikosi
cha leo cha Simba kitakacho kuwa kikicheza dhidi ya Mtibwa Sugar kutokana na
kwamba bado yuko katika uangalizi wa daktari wa Simba.
Hata hivyo Kamwaga amesema huenda mchezaji huyo
akaanza kuingia dimbani katika mchezo wa marudiano dhidi ya FC Libolo ya Angola
mchezo utakaochezwa Machi 2 jijini Luanda.
Mussa Mudde ambaye alikuwa kwao nchini Kenya
amerejea jana na kujiunga na kambi ya klabu ya Simba.
Mudde alikwenda kwao kwa ajili ya kushiriki mazishi
ya mwanae.
Hata hivyo nafasi ya Mudde kucheza mchezo wa leo
dhidi ya Mtibwa haipo kufuatia uongozi wa Simba kumpa chaguo kama angependelea
kufanya hivyo ama la kwa kuwa suala la kufiwa na mtoto lipewa uzito mkubwa na
uongozi huo.
No comments:
Post a Comment