Luis Suarez
usiku wa jana alikuwa nyota wa mchezo wa hatua ya timu nane za mwisho za
michuano ya Ulaya (Europa League) ambapo alichangia kwa sehemu kubwa ushindi wa
Liverpool wa mabao 3-1 dhidi ya Zenit lakini mshambuliaji huyo kwa mara nyingine
tena ameingia katika gumzo lingine ambalo linaweza kumpelekea kuadhibiwa na
shirikisho la soka barani Ulaya EUFA.
Licha ya ushindi huo wa Liverpool wa mabao 3-1 bado
haikutosha kuisogeza mbele timu hiyo kufuatia matokeo hayo kufanya kuwepo
matokeo ya sare ya mabao 3-3 lakini Zenit wakifaidika na bao la
ugenini.
Hata hivyo wekundu hao wanaweza pia wakapata pigo
lingine la pili endapo UEFA wataamua kumuadhibu Luis Suarez raia wa Uruguay
kufuatia kumtimba katika kipindi cha Tomas Hubocan katika mchezo
huo.
Luis Suarez akimtimba
makalio Tomas Hubocan wa Zenit.
Mlinzi huyo alikuwa
akiukimbia mpira kujaribu kuepuka mpira wa kurushwa upande wao na ndipo
alipodondoka akiwa katika kukabiliana na Suarez ambaye kwa makusudi alimkanyaga
kwa makusudi.
No comments:
Post a Comment