MABINGWA wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga wamefungwa
mabao 2-1 na timu ya Augsburg inanayocheza Ligi Kuu ya Ujerumani kwenye
michuano ya Mpumalanga katika Uwanja wa Mbombela, Afrika Kusini leo.
Bao pekee la Yanga lilifungwa na mshambuliaji mpya wa
timu hiyo Jean Baleke akimalizia kwa kichwa krosi iliyopigwa na Maxi Nzengeli
katika dakika ya 87.
Augsburg walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 37
likifungwa na Mads Pederson kabla ya Philip Titz kufunga bao la pili dakika ya
81.
Huo ni mchezo wa kwanza katika michuano hiyo
inayohusisha timu tatu ambazo ni Yanga, Augsburg kutoka Ujerumani na Tx Galaxy
ya Afrika Kusini.
Mchezo wa pili wa michuano hiyo Yanga watacheza dhidi
ya Tx Gallaxy, Julai 24, mwaka huu.
Timu hiyo yenye maskani yake mitaa ya Twiga na
Jangwani Dar es Salaam, watamaliza ziara yao Julai 28 ambapo watacheza dhidi ya
Kaizer Chiefs kwenye michuano ya Toyota Cup.
Aidha, Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi aliutumia
mchezo huo kuwajaribu wachezaji wake wapya waliosajiliwa kwa ajili ya msimu
ujao.
Waliosajiliwa msimu huu ni Clatous Chama, Jean Baleke,
Price Dube, Duke Abuya, Aziz Andabilwe, Chadack Boka na Khomeini Abubakar.
No comments:
Post a Comment