Mkufunzi Ibrahim Kidiwa akizungumza na wachezaji wa Kituo cha Sky Force cha jijini Tanga hivi karibuni |
Na Rahel Pallangyo
KITUO cha kukuza na kulea vipaji vya soka cha Sky
Force cha jijini Tanga kimeomba wadau kuwasaidia vifaa vya michezo.
Kituo hicho chenye wachezaji 167 wenye umri wa kuanzia
miaka 9-20 kinakabiliwa na uhaba wa vifaa vya kuchezea ikiwemo bips, koni,
mipira na jezi wanafanyia mazoezi Uwanja wa Shule ya Sekondari Magaoni (Japan).
Mmoja wa wamiliki wa kituo hicho, Kombo Abdallah
alisema yeye na wenzake Fakhi Amour na Ibrahim Kidiwa walianzisha kituo hicho
kutokana na mapenzi makubwa waliyonayo katika mchezo wa soka.
“Tulianzisha kituo hiki kutokana na mapenzi yetu ya
dhati kwa mchezo wa soka lakini kutokana na kipato chetu kuwa cha kawaida
tunashindwa kumudu baadhi ya gharama za uendeshaji, hivyo tunaomba wadau
watusaidie,” alisema Kombo.
Kombo alisema wachezaji wote wanafundishwa bure bila
malipo yoyote na wamefanya hivyo kwa ajili ya kuwasaidia vijana kupata msingi
mzuri wa soka.
Aidha, alisema pia wanafundisha vijana wanaopenda
kuwa waamuzi wa soka na tayari wengine wameanza kuchezesha Ligi Daraja la Tatu
Mkoa wa Tanga.
Timu ya kituo hicho kinashiriki ligi ya vijana chini
ya umri wa miaka 17 ya Mkoa wa Tanga na inashika nafasi ya saba kati ya timu 14
ikiwa na pointi nne huku vinara Fair Play ikiongoza kwa pointi tisa sawa na TFF
Centre.
No comments:
Post a Comment