Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, April 3, 2018

WEMA NA GABO WALIVYONG'ARA TUZO ZA FILAMU ZA SINEMA ZETU









WAIGIZAJI wa Tanzania, Wema Sepetu na Salim Ahmed ‘Gabo’ juzi waliwatoa kimasomaso Watanzania baada ya kuibuka waigizaji bora katika tuzo za filamu za Sinema Zetu International Film Festival Award (SZIFF) zilizofanyika katika ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam
Katika filamu hizo ambazo zilikuwa na vipengele 19 ambavyo vilikuwa vinawania kimoja kikiwa kipengele cha chaguo la watu ambapo Gabo alichukua tuzo tano na Wema Sepetu aliondoka na tuzo mbili na filamu ya ‘Binti Zanzibar’ kutoka Zanzibar ikiondoka na tuzo tatu.
Gabo ambaye aliingiza filamu ya Safari ya Gwalu aliondoka na tuzo ya mwigizaji bora wa kiume ambapo pia Safari ya Gwalu ilipata tuzo ya filamu bora, skiripti bora, muziki bora wa filamu pia ikapata tuzo ya mwongozaji bora, (Daniel Manege)
Wema alipata tuzo ya mwigizaji bora wa kike na filamu yake ya Heaven Sent ikapata tuzo ya watazamaji kwani ilipigiwa kura na watazamaji.
Filamu ya binti Zanzibar iliondoka na filamu tatu katika vipengele vya filamu fupi bora, best Screen Play na Best Original Music (Abdallah Marash)
 Mchekeshaji bora alikuwa Musa Kitale, mhariri bora wa filamu Soudy Visual (Usinitege), mwongozaji bora wa filamu Said Abdallah (Picha) na sinematografia bora ni Usinitege iliyotengenezwa na Soudy Visual
Filamu bora ni malipo duni kwa wapagazi na mwongozaji bora ni Anwar Msechu kupitia filamu ya malipo duni kwa wapagazi
Filamu ya Watatu kutoka Kenya iliondoka na tuzo ya mhariri bora wa filamu na  sinematografia bora.
Akizungumza baada ya kukabidhi tuzo mgeni rasmi Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dk. Jakaya Kikwete ambaye aliwataka wasanii kutumia fursa hiyo kutengeneza kazi nzuri ambazo zitaweza kushindana kimataifa na kuacha kuiga wasanii wa nje.
Tuzo hizo zilihudhuriwa na wasanii na watu maarufu wengi akiwemo mwigizaji kutoka India aitwaye Pritika Rao maarufu kama Aliyah ambaye amejizolea umaarufu kupitia tamthilia ya ‘Beitehaa’ Mzee Majuto, Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Michezo na Utamaduni Juliana Shonza na Katibu Mkuu wa bodi ya filamu Joyce Fissoo
Mchakato wa kupata mshindi wa tuzo hizo ulianza Oktoba mwaka 2017 ambapo mwigizaji Elizabeth Michael ‘Lulu‘ alichaguliwa kuwa balozi wa (SZIFF) Sinema Zetu International Festival kwa mwaka 2017/2018.

No comments:

Post a Comment