Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, April 3, 2018

MASOGANGE AHUKUMIWA MIAKA MIWILI AU FAINI SHILINGI MILIONI 1.5

Related image
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo hii imemhukumu kwenda jela miaka miwli au kulipa faini ya Shilingi milioni 1.5, Video Queen Agnes Gerald maarufu kwa jina la Masogange kwa kosa la kutumia dawa za kulevya aina ya Heroin.

Video Queen huyo aliyeanza kutamba baada ya kuonekana katika video ya msanii wa Bongo Fleva, Belle 9 katika wimbo uliojulikana kwa jina la Masogange sakata lake liliibuliwa na mkuu wa mkoa wa Dar es salaam alipowataja watu maarufu kufika Polisi kwa kujihusisha matumizi ya dawa za kulevya mwezi Februari mwaka jana.

No comments:

Post a Comment