Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, March 31, 2018

NGORONGORO HEROES YATOKA SARE NA DR CONGO TAIFA







TIMU ya taifa ya Tanzania kwa wachezaji wenye umri chini ya miaka 20, Ngorongoro Heroes, leo imeshindwa kutumia uwanja wake wa nyumbani baada ya kulazimishwa suluhu dhidi na wenzao wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Katika pambano hilo la kusaka kufuzu kucheza fainali za Mataifa ya Afrika zitakazofanyika mwakani Niger, Ngorongoro Heroes pamoja na kupata kona nyingi,  ilishindwa kabisa kuzifumania nyavu za wapinzani wao hao kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
Kwa matokeo hayo, Ngorongoro Heroes sasa inahitaji sare ya kuanzia angalau bao 1-1 au ushindi wa aina yoyote ili kusonga mbele, hatua ambayo itakutana na Mali katika mbio za kusaka kucheza fainali hizo kwa mara ya kwanza.
Kocha wa Ngorongoro Heroes, Ammy Ninje amesema kuwa ataongeza dozi kwa wachezaji wake ili kuhakikisha wanafanya vizuri katika mchezo wa marudiano nchini Congo.
Naye Nahodha wa timu hiyo, Said Bakari alisema kuwa walipata nafasi nyingi lakini bahati mbaya walishindwa kuzitendea haki, lakini mchezo ujao watajitahidi kuhakikisha wanaibuka na ushindi na kusonga mbele hatua inayofuata.
Ngorongoro walipata kona 11 dhidi ya tatu za Congo, ambazo hazikuwasaidia kuibuka japo na ushindi kiduchu.
Katika dakika 45 za kwanza, timu zote ziliweza kutengeneza nafasi, lakini zilishindwa kupata mabao na hivyo kwenda mapumziko zikiwa hazijafungana.
Kikosi cha Ngorongoro Heroes: Ramadhani Kabwili, Kibwana shomary, Nickson Kibabage, Ally Msengi, Dickson Job, Ally Ngazi, Assadi Juma, Kelvin Naftai, Paul Peter/Riphat Msuya, Abdul Seleman na Said Bakari/Mohamed Mussa.

No comments:

Post a Comment