Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, April 4, 2018

TWIGA STARS YALAZIMISHWA SARE YA MABAO 3-3 NA SHEPOLOPOLO TAIFA




TIMU ya Taifa ya Soka ya Wanawake ya Twiga Stars imeshindwa kuutumia vizuri uwanja wao wa nyumbani baada ya kulazimishwa sare ya kufungana mabao 3-3 na wenzao wa Zambia, katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Mchezo huo ni kwa ajili ya kufuzu kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika zitakazofanyika Ghana baadaye mwaka huu.
Twiga Stars iliandika bao la kwanza katika kipindi cha kwanza baada ya Stumai Abdallah kufunga bao na kuifanya timu hiyo kuwa mbele baada ya kupokea pasi ya Asha Rashid.
Twiga Stars iliandika bao la pili kupitia kwa Asha Rashid aliyefunga katika dakika ya 22 baada ya kuiwahi krosi ya chini chini iliyochongwa na Stumai Abdallah.
Dakika tano baadaye, Zambia waliandika bao la pili kupitia kwa mshambuliaji wao hatari Barbra Banda katika dakika ya 27 kabla ya timu hiyo haijasawazisha katika dakika ya 49 kupitia kwa Misozi Zulu.
Twiga Stars ilipata bao la tatu lililofungwa na Asha Rashid katika dakika ya 47 kwa shuti kali lililomshinda kipa wa timu ya taifa ya Zambia, Catherune Chileshe.
Zambia walisawazisha kupitia kwa mchezaji wao hatari, Banda baada ya kuwapiga chenga karibu mabeki wanne wa Twiga Stars na kuujaza mpira kimiani.
Kikosi cha Tanzania: Fatuma Omary, Wema Richard, Happy Hezron, Fatuma Issa, Sophia Mwasikili/Ester Mayala, Everline Sekikubo, Stumai Abdallah, Donisia Daniel, Asha Rashid, Mwanahamisi Omary na Amina Ally.

No comments:

Post a Comment