Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, April 5, 2018

LIGI YA MABINGWA KUANZA MEI MOSI KATIKA VITUO VINNE


LIGI ya mabingwa wa mikoa inatarajiwa kuanza Mei Mosi hadi Mei 18 na imepangwa kufanyika katika vituo vinne na itashirikisha timu 28.
Akizungumza na wandishi wa habari leo, Mkurugenzi wa Mashindano wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Efrem August alisema ligi hiyo itachezwa katika vituo vya Kilimanjaro, Rukwa, Singida, na Geita.
“Mikoa ya Geita, Kilimanjaro, Singida na Rukwa ndio itakuwa mwenyeji wa vituo na kila kituo kitakuwa na timu saba. Pia hii mikoa ambayo imepata wenyeji ilikubali kugharamia malazi na chakula kwa waamuzi, kamishna na wasimamizi wa vituo,” alisem Efrem.
Kituo D cha Kilimanjaro kitakuwa na timu za Karume Market ya Dar es Salaam, Sahare ya Tanga, Bishop Durning Sports ya Arusha, Usalama Sports Club ya Manyara, Stand FC ya Pwani, Moro Kids ya Morogoro na Uzunguni FC ya Kilimanjaro
Kituo C cha Singida kitakuwa na timu za Gwassa Sports ya Dodoma, Iringa United ya Iringa, Kipagalo FC ya Njombe, Temeke Market ya Dar es Salaam, Majimaji Rangers ya Lindi, Mwena FC ya Mtwara na wenyeji Stand Dortmund ya Singida.
Kituo B cha Rukwa kitakuwa na timu za Watu FC ya Katavi, Laela FC ya Rukwa, Tukuyu stars ya Mbeya, Red Stars FC ya Kigoma, Tabora FC ya Tabora, Black Belt ya Ruvuma na Migombani FC ya Songwe  
Kituo A kitakuwa Geita na timu za Ungindoni ya Dar es Salaam, Kumunyange FC ya Kagera, Fathom FC ya Mwanza,Zimamoto FC ya Shinyanga, Nyamongo ya Mara, Gipco FC ya Geita na Ambassador FC  ya Simiyu.
Usajili ulifungwa jana  na Aprili 24 kutafanyika kikao cha kamati ya Sheria na Hadhi za wachezaji  baada ya kamati ua usajili na pingamizi kukutana Aprili 18

No comments:

Post a Comment