Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, April 18, 2018

PICHA ZA UTUPU ZAWAFIKISHA KWA PILATO DIAMOND NA NANDY


Diamond Platnumz
WAZIRI wa Habari, Sanaa, Utamduni na michezo, Dk Harrison Mwakyembe ameagiza kukamatwa kwa wasanii wa muziki wa kizazi kipya  Faustina Charles ‘Nandy’ na Nasib Abul ‘Diamond’ baada ya kusambaa kwa video zake chafu na kufikishwa kituo cha polisi kwa ajili ya mahojiano na uchunguzi zaidi.
Kauli hiyo imekuja baada ya Mbunge wa jimbo la Ulanga,  Morogoro, Goodluck Mlingwa  kuuliza ni hatua gani za serikali zimechukuliwa ili kupambana na wasanii wanaweka picha za uchi na matusi katika mitandao.
Dk.Mwakyembe amethibitisha kuwa msanii Diamond bado yuko polisi alikofikishwa tangu juzi kwa ajili ya mahojiano baaada ya kuvujisha video akiwa na wanawake tofauti faragha.
Aidha Dk. Mwakyembe alisema Nandy naye atahojiwa na polisi kufuatia video yake ya faragha akiwa na msanii mwenzake Billnass kusambaa mitandaoni.
“Tulitunga sheria mwaka 2010 lakini tulikosa sheria za kubana wasanii  katika maudhui hasa katika upande wa mitandao, tumeshatunga hizo kanuni na sasa zimeanza kufanya kazi,”
”Kuna baadhi ya vijana wamekuwa wakifanya uhuni uhuni katika mitandao ya kijamii sana na tumeanza kuwafanyia kazi , yupo msanii Diamond ambaye  amefikishwa polisi tangu jana (juzi) kutokana na kusambaa kwa picha zake chafu, hata hivyo pia binti Nandy pia inabidi akamatwe ahojiwe,” alisema Dk Mwakyembe.

No comments:

Post a Comment