Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, April 18, 2018

MONALISA KUPELEKA TUZO YAKE BUNGENI


MWIGIZAJI Yvonne Cherrie 'Monalisa’ ambaye amepata tuzo ya mwigizaji bora Afrika zinazotolewa na The African Prestigious Awards' nchini Ghana juzi anatarajiwa kuipeleka tuzo hiyo bungeni ikiwa ni nembo ya ushindi wa taifa.
Katika tuzo hizo mwizagizaji Ray Kigosi aliibuka mwigizaji bora wa kiume na  mpigapicha mahiri alikuwa Moiz Hussein wa Tanzania pia huku Rais Dk John Pombe Magufuli  akaipata kwa upande wa viongozi bora Afrika.
Akizungumza jana mama mzazi wa Monalisa anayeitwa Natasha Lewis  alisema  baada ya Monalisa kurudi kutoka Accra Ghana anatarajiwa kwenda Dodoma kwa ajili ya kuipeleka tuzo hiyo bungeni.
Naye Monalisa kupitia ukurasa wake wa Instagram aliwashukuru Watanzania wote kwani ni zaidi ya miaka 19 sasa akiwa kwenye sanaa na wamekuwa nyuma yake na tuzo aliyoipata ni kwa ajili yao kwani bila mashabiki isingewezekana.
Wakati huo huo Ray Kigosi amesema alishindwa kuhudhuria tuzo hizo kwa sababu alikuwa nje kikazi
“Sikufanikiwa kuhudhuria kwenye tuzo hizo kwa sababu nikuwa Afrika Kusini kikazi sina cha kuwalipa ndugu zangu zaidi ya kuendelea kuwaletea kazi nzuri zenye viwango bora ili tuendelee kuiletea heshima nchi yetu,” alisema Ray Kigosi
Tuzo hizo zilizotolewa usiku wa kuamkia April 15, 2018 mjini Accra nchini Ghana, Ray na Monalisa waliibuka washindi kutoka Tanzania.