Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, January 17, 2018

YANGA YAKUBALI MUZIKI WA MWADUI FC NYUMBANI, YASULUHU



MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga leo wamepunguzwa kasi baada ya kulazimishwa suluhu na Mwadui ya Shinyanga katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Kwa sare hiyo, Yanga imeendelea kupiga kwata katika nafasi ya tano ya msimamo wa ligi hiyo ikiwa na pointi 22, moja nyuma ya Singida United iliyopo katika nafasi ya nne.
Simba na Azam FC ambazo zinashika nafasi ya kwanza na pili kila moja ikiwa na pointi 26, kesho zina nafasi ya kuzidi kuikimbia Yanga endapo zitashinda mechi zao.
Simba wanacheza dhidi ya Singida jijini Dar es Salaam wakati Azam FC watatoana jasho dhidi ya Majimaji ya Songea mjini humo.
Katika mchezo huo wa jana, Yanga nusura ipate bao katika dakika ya 23, kupitia kwa Emmanuel Martin baada ya kuingia ndani ya 18, lakini kabla hajaleta madhara, mabeki wa Mwadui walifanikiwa kumdhibiti.
Dakika ya 32, Amis Tambwe alipata nafasi nzuri ya kufunga, lakini alipiga mpira pembeni kabla Paul Nonga hajashindwa kufunga katika dakika ya 33 baada ya kupiga shuti lililodakwa na kipa wa Yanga, Youthe Rostand.
Mashabiki wa Yanga hawakufurahishwa na matokeo hayo, ambapo baadhi yao walipiga kelele kuwa hawamtaki kocha msaidizi wa timu hiyo, Shadrack Nsajigwa.
Nsajigwa amekuwa akikaa katika benchi la timu hiyo baada ya kocha mkuu, George Lwandamina wa Zambia kwenda kwao kwa ajili ya msiba wa mtoto wake.
Hata hivyo, Lwandamina amesharejea nchini na jana alikuwepo jukwaani kwenye Uwanja wa Uhuru wakati Yanga ikicheza na Mwadui.
Vikosi vilikuwa Yanga: Youthe Rostand, Hassan Kessy, Mwinyi Haji, Andrew Vicent, Kelvin Yondan, Said Juma, Juma Mahadhi, Pius Buswita, Amis Tambwe, Ibrahim Ajibu na Emmanuel Martun.

Mwadui: Anord Massawe, Jackson Salvatory, David Luhende, Joram Mgeveke, Idd Mfaume, Awadhi Juma, Jean Girukwishako, Abdallah Omary, Paul Nonga, Evangestus Bernard na Awese Awese.

No comments:

Post a Comment