Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, January 17, 2018

OKWI AWAANGUKIA WACHEZAJI WENZAKE NA MASHABIKI

Image result for okwi
WAKATI Simba ikishuka dimbani kesho, mshambuliaji wake, Emmanuel Okwi ameomba radhi wachezaji wenzake, viongozi na benchi la ufundi baada ya kukosekana kwenye kikosi kwa muda mrefu bila sababu za msingi.
Simba kesho inashuka dimbani jijini Dar es Salaam kucheza dhidi ya Singida United katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Akizungumza Kocha wa Simba, Masoud Djuma alisema amemsamehe Emmanuel Okwi, kwani aliomba radhi kwake, kwa uongozi na wachezaji wenzake na juzi alianza rasmi mazoezi na timu.
“Unajua binadamu hakuna aliyekamilika cha lazima ni muunganiko wa pamoja, tukianza kunyoosheana vidole nguvu inapungua cha lazima ni kurudisha nidhamu kwenye timu. Hakuna mchezaji au mtu yeyote ambaye yuko juu ya timu, hata rais wa timu hayuko juu ya timu, timu inakuja kwanza halafu mtu baadaye,” alisema Masoud.
Pia Masoud amemuombea radhi Emmanuel Okwi kwa mashabiki, akiwataka kuungana ili timu ifanye vizuri katika mchezo wa leo dhidi ya Singida United na michezo ijayo.
Simba ambayo ilikuwa imeweka kambi mkoani Morogoro ilirejea Dar es Salaam kwa ajili ya mchezo wa leo dhidi Singida United utakaochezwa kwenye wa Taifa.
Mchezo huo unachezwa kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam baada ya serikali kuruhusu kutumika kwa mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara na zile za kimataifa zilizo chini ya Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF).
Baada ya mchezo leo, Yanga watautumia Jumapili watakapokabiliana na Ruvu Shooting, kwani umeruhusiwa kutumika mara moja pekee kwa wiki.

Serikali iliufungia uwanja huo tangu Septemba mwaka jana kwa ajili ya matengenezo ambayo tayari yamekamilika.

No comments:

Post a Comment