Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, January 16, 2018

Chirwa afungiwa mechi tatu na faini ya 500,000

Kamati ya nidhamu iliyokutana Jumapili Januari 14, 2018 imepitia kesi ya mshambuliaji wa Yanga Obrey Chirwa iliyowasilishwa na Bodi ya Ligi iliyohusu mchezo namba 83 kati ya Yanga na Tanzania Prisons iliyochezwa Novemba 25, 2017 Uwanja wa Azam Complex.

Chirwa alishtakiwa kwa kosa la kumpiga mchezaji wa Tanzania Prisons kwenye mchezo huo uliomalizika kwa sare ya kufungana bao 1-1.

Chirwa ambaye alifika kusikiliza kesi hiyo akiwa na muwakilishi wake alikiri kutenda kosa hilo.

Kamati baada ya kumsikiliza Chirwa na kupitia Video za mchezo huo pamoja na taarifa ya kamishna  na Muamuzi imetoa adhabu kwa mchezaji huyo kupitia Kanuni za Ligi Kuu kanuni ya 37(7b) na kanuni za nidhamu za TFF kifungu cha 48(1d) na 48(2).


Chirwa amefungiwa mechi tatu(3) na kutozwa faini ya shilingi laki tano(500,000)