Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, November 21, 2017

USHINDANI WA KIATU CHA DHAHABU WANOGA

UNAWEZA kusema ushindani wa kuwania kiatu cha dhahabu kwa Ligi Kuu Tanzania Bara, umeanza baada ya mshambuliaji wa Yanga Obrey Chirwa kufikisha mabao sita akiwa nyuma ya mshambuliaji wa Simba Emanuel Okwi kwa  mabao mawili.
Okwi anaongoza akiwa na mabao nane, katika mechi nane za ligi kuu alizocheza msimu huu wakati Chirwa amecheza mechi tisa.
Mchezaji wa Mohamed Rashid wa Tanzania Prisons pia ana mabao sita sawa na Chirwa huku Ibrahim Ajib wa Yanga akiwa na mabao matano sawa na Ramadhan Kichuya wa Simba na Habibu Kiyombo wa Mbao FC.
Kwa mtazamo wa haraka wachezaji wote hawa wanaweza kuibuka mfuungaji bora mwishoni mwa msimu endapo wataendelea na kasi hii.
Obrey Chirwa baada ya mchezo dhidi ya Mbeya City juzi alisema kiatu cha dhahabu msimu huu ni cha kwake.
“Mimi ndio nitakuwa mfungaji bora kwasababu nilianza ligi vibaya lakini sasa mpira umetulia mguuni, nitaendelea kufunga kwani ushirikiano na wachezaji wenzangu ni mzuri,” alisema Chirwa.

Katika mchezo wa juzi Obrey Chirwa alifunga hat trick ya pili tangu ligi kuu msimu huu uanze baada ya ile ya Okwi aliyofunga dhidi ya Ruvu Shooting.

No comments:

Post a Comment