Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, November 21, 2017

OMOG: MO HAUZWI NG'O

KOCHA Mkuu wa Simba, Joseph Omog amesema Mohammed Ibrahim ni mmoja kati ya wachezaji anaowahitaji zaidi katika kikosi chake hayupo tayari kumuona akiondoka.
Kauli ya Omog imekuja baada tetesi kuenea kuwa Yanga wapo kwenye harakati za kumuwinda baada ya dirisha dogo la usajili kufunguliwa.
“Kama kuna timu yoyote inamhitaji Mo kwa sasa hawezi kuondoka, bado tunamhitaji zaidi katika kikosi chetu na nimeshawaambia viongozi,”
“Nilikuwa simtumii kwa sababu alikuwa majeruhi ila sasa amepona na  nimeanza kumtumia na anafanya vizuri hivyo sipo tayari kuona akiondoka wanaomtaka wasubiri lakini siyo sasa,” alisema Omog.
Naye Ibrahim aliandika kwenye ukurasa wake wa instagram kuwa bado ni mali ya Simba kwani ana mkataba wa mwaka mmoja.

“Mimi bado ni mali ya Simba bado nina mkataba wa mwaka mmoja,” aliandika Ibrahim.

No comments:

Post a Comment