Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, November 23, 2017

SIMBA DHIDI YA LIPULI KUCHEZWA UHURU


MCHEZO wa Ligi Kuu Tanzania dhidi ya Simba na Lipuli sasa utachezwa kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam badala ya Uwanja wa Azam Complex.
Awali mechi hiyo ilihamishiwa Azam Complex baada ya wamiliki wa Uwanja wa Uhuru kueleza kuwa utakuwa na matumizi mengine Novemba 26, 2017.
Akizungumza leo Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi, Boniface Wambura alisema michezo ya Novemba 25 na 26 ililazimika kuhamishwa kutokana na Uwanja wa Uhuru kuwa na matumizi mengine lakini serikali imewarusu kutumia uwanja huo siku ya Jumapili.
“Mechi ya Yanga dhidi ya Tanzania Prisons itachezwa Chamazi ila mchezo wa Simba dhidi ya Lipuli wao watacheza uwanja wa Uhuru kwani serikali imeturuhusu kuutumia siku ya Jumapili,” alisema Wambura.
Simba ambayo imetoka kucheza ugenini na kufanikiwa kuvuna pointi sita inayoongoza ligi ikiwa na pointi 22 huku Lipuli ikiwa na pointi 13 katika nafasi ya saba.


No comments:

Post a Comment