Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, November 21, 2017

PASTORY ATHANAS KURUDI STAND UNITED KWA MKOPO

KUTOKANA na ushindani wa namba uliopo kwenye klabu ya Singida United kocha Hans Pluijm amekubali kumtoa kwa mkopo mshambuliaji wake Pastory Athanas, kwenda Stand United
Akizungumza Kocha Hans Pluijm alisema amekubali maombi ya Stand United, kwa sababu mchezaji huyo amekuwa hapati nafasi tangu walipomsajili mwanzoni mwa msimu huu akitokea Simba.
“Nimekubali Athanas aondoke ili kulinda kipaji kwasababu mchezaji asipopata nafasi ya kucheza kiwango kitashuka,” alisema Pluijm.
Athanas ametolewa kwa mkopo na uongozi wa Singida United unasema umekubaliana na Simba na umefanya kwa faida ya pande zote tatu, yaani Simba, Singida na mchezaji mwenyewe.
Katibu Mkuu wa Stand United, Kenedy Mwangi alikiri kufanya usajili wa wachezaji wanne, watatu wa kimataifa na mmoja ni Athanas lakini akakataa kuwataja majina kwa kuhofia kutibuliwa kwa vile kuna taratibu hazijakamilika.

“Tumejipanga kusajili wachezaji wanne, wawili Warundi, Mganda mmoja na Mtanzania mmoja ambao wanacheza namba tano, nane na tisa, baadhi ya taratibu zimekamilika na nyingine bado hivyo zikikamilika tutaweka majina yao hadharani,” alisema Mwangi 

No comments:

Post a Comment