Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, November 21, 2017

SASII, MFAUME NA LILA KUCHEZESHA CECAFA

WAAMUZI watatu wa Kimataifa wa Tanzania wameteuliwa kuchezesha mashindano ya Chalenji yanayotarajiwa kufanyika Nairobi Kenya kuanzia Desemba 3-17.
Akizungumza na Katibu Mkuu wa Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) ambao ndio waandaji wa mashindano hayo aliwataja waamuzi hao kuwa ni Elly Sasii, Nassor Mfaume na mwamuzi msaidizi Soud Lila.
“Waamuzi watakaochezesha Chalenji wapo 16, nane waamuzi wa kati na nane waamuzi wasaidizi na watatu wanatoka Tanzania. Septemba 29 wanatakiwa kuwa wamefika Nairobi kwani Septemba 30 na Desemba Mosi watafanya mtihani wa utimamu,” alisema Musonye.
Waamuzi wengine ni George Gotagota na Abdoul Karim (Burundi), Peter Waweru na Anthony Ogwayo (Kenya), Alex Muhabi (Uganda) na Malong Akech (Sudan Kusini)
Waamuzi wasaidizi ni Herve Kakunze (Burundi), Tigle Belachew (Ethiopia), Ndagijimana Theogene (Rwanda), Tony Kidiya na Joshua Achila (Kenya), Dick Okello na Ronald Katenya (Uganda)
Mashindano ya Chalenji yanatashirikisha timu kumi ambazo ni Tanzania, Zanzibar, Uganda, Somalia, Sudan, Ethiopia, Sudan Kusini, Burundi, Rwanda na wenyeji Kenya.




No comments:

Post a Comment