Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, November 8, 2017

SAMATTA KUIKOSA BENIN

Taarifa kutoka kwa matatibu wa Genk ya Ubelgiji, zinasema kwamba Mbwana Samatta anatarajiwa kufanyiwa upasuaji mdogo na mpaka kupona, madaktari wamesema itamchukua wiki nane ili kurejea uwanjani.
Kocha wa Taifa Stars, Salum Shabani Mayanga amepokea taarifa hiyo na kusema haijawa bahati kwa Stars, lakini atapanga kikosi chake vema kwa wachezaji atakaokuwa huko Benin akiwamo Abdi Banda na Farid Mussa.
Wachezaji watakaosafiri ni Aishi Manula, Peter Manyika, Gadiel Michael, Boniphas Maganga, Kelvin Yondani, Nurdin Chona, Himid Mao, Hamis Abdallah, Raphael Daudi, Mohamed Issa, Jonas Mkude, Mudathir Yahya, Simon Msuva, Shiza Kichuya, Faridi Mussa,  Ibrahim Ajib, Mbaraka Yusuph na Elias Maguli

No comments:

Post a Comment