Straika wa Chelsea Diego Costa amefungiwa Mechi 3 na FA, Chama cha Soka England, baada ya kupatikana na hati ya kumpiga Beki wa Arsenal Laurent Koscielny huku Beki wa Arsenal Gabriel akifutiwa Kadi Nyekundu aliyopewa.
Tukio hilo lilitokea Jumamosi iliyopita na halikuonwa na Refa Mike Dean lakini muda fupi baadae akamtoa kwa Kadi Nyekundu Beki wa Arsenal Gabriel Paulista.
Mara baada ya Adhabu hiyo kutolewa hapo Jana Klabu ya Chelsea ilitoa taarifa na kusema imesikitishwa na uamuzi huo.
Costa, mwenye Miaka 26, alimsukuma kwa mkono usoni Beki wa Arsenal Laurent Koscielny na pia kumwangusha chini na baada ya hapo kuvaana na Beki mwingine wa Arsenal, Gabriel Paulista, ambae alitolewa nje kwa Kadi Nyekundu kwa kumpiga Teke Costa.
Mechi ambazo atazikosa Costa ni zile za Chelsea dhidi ya Walsall, kwenye Capital One Cup, na za Ligi Kuu England dhidi ya Newcastle na Southampton.
Pia, FA imeamua kuifuta Kadi Nyekundu kwa Gabriel baada ya Arsenal kukata Rufaa na sasa yuko huru kucheza Mechi.
Mbali ya Costa, pia Klabu zote mbili zitapanda kizimbani kujibu Shitaka la kushindwa kuzuia Wachezaji wao kuleta vurugu na zimepewa hadi Alhamisi Septemba 24 kujibu Mashitaka yao.
Juzi, FA ilitoa ufafanuzi kwa nini ilimfungulia Mashitaka Costa kwa kusema tukio lake halikuonwa na Refa Mike Dean hivyo likapelekwa kwa Marefa Watatu wa zamani ambao waliupitia Mkanda wa tukio na wote waliafiki alipaswa kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu.
Diego Costa kwenye majanga yake dhidi ya Laurent Koscielny ndani ya boxMITANANGE 3 ATAKAZOKOSA DIEGO COSTA:
No comments:
Post a Comment