Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, November 18, 2017

KOCHA NINJE AITA 20 KWA AJILI YA CHALENJI


KOCHA Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Stars’, Ammy Ninje ametangaza kikosi cha wachezaji 20 ambao wanatarajia kuingia kambini Novemba 26 kwa ajili ya kujiandaa na mashindano ya Chalenji yatakayofanyika nchini Kenya.
Akizungumza leo Ninje ambaye aliteuliwa jana kushika mikoba hiyo alisema atakuwa anafundisha darasani na baadae kwa vitendo uwanjani ili kuwapa wepesi wachezaji kuelewa.
“Nitakuwa naangalia katika maadili ya timu, nitaongea na wachezaji na kuwaeleza kuwa timu ya Taifa ni kuwa balozi ili kuwabadilisha mtazamo,” alisema Ninje.
“Kikosi hiki nimeshirikiana na Kocha wa Taifa Stars Salum Mayanga kwasababu mimi nina muda wa miezi mitatu tangu niwe kwenye benchi la Taifa Stars,” aliongeza Ninje.
Pia Ninje alisema anataka kuwasaidia wachezaji kisaikolojia ili waende mbele kimpira kwasababu Argentina na Brazil wana maisha magumu kama Tanzania lakini wapo wanacheza soka Ulaya.
Aidha alisema anapenda wachezaji ambao wanapenda kujifunza na wapo tayari kujifunza
Kikosi hicho kinaundwa na makipa Aishi Manula (Simba), na Peter Manyika (Singida United).
Walinzi ni Gadiel Michael na Kelvin Yondani (Yanga), Bonipha Maganga (Mbao FC), Kennedy Juma (Singida United), Mohammed Hussein na Erasto Nyoni (Simba) 
Viungo wa kati ni Himid Mao (Azam FC) ambaye atakuwa nahodha, Hamis Abdallah (Sony Sugar/Kenya), Mzamiru Yassin (Simba) na Raphael Daud (Yanga).
Viungo wa pembeni ni Shizza Kichuya na Jonas Mkude (Simba), Abdul Hilal (Tusker/Kenya), Ibrahim Ajib (Yanga) na washambuliaji ni Elias Maguli (mchezaji huru), Mbaraka Yussuph (Azam FC), Danny Lyanga (Fanja Oman) na Yohana Mkomola (mchezaji huru). 
Benchi la ufundi linaundwa yeye NinjeKocha Mkuu, Fulgence Novatus (Kocha Msaidizi), Patrick Mwangata (Kocha wa makipa), Danny Msangi (Meneja), madaktari ni Richard Yomba na Gilbert Kigadye na Ally Ruvu (Mtunza Vifaa).

mashindano ya Chalenji kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) yanatarajiwa kuanza Desemba 3-17 , Nairobi Kenya na Kilimanjaro Stars imepangwa kundi A pamoja na timu za Libya, Rwanda na  wenyeji Kenya

No comments:

Post a Comment