SHIRIKISHO
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko taarifa za vifo vya
wanafamilia wawili wa soka vilivyotokea Oktoba 5, 2017 kwa nyakati tofauti.
Akizungumza
Ofisa habari wa TFF Alfred Lucas alisema Rais wa TFF Wallace Karia amesikitishwa
na taarifa aliyekuwa mchezaji wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Zanzibar ‘Zanzibar Heroes’, pamoja na Afrika
Mashariki miaka ya 1950 na 1960, Abdul Majham na Mwamuzi wa Daraja la Kwanza
Mirambo Tshikungu.
“Hakika
nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za vifo hivi. Ni mshtuko mkubwa sana
katika familia ya mpira wa miguu hapa Tanzania, natambua pia ni majonzi makubwa
kwa familia za marehemu,” alisema Rais Karia.
“Familia,
ndugu, jamaa, marafiki, majirani wawe na moyo wa subira baada ya ndugu zetu
kutangulia mbele ya haki. Kwa kuwa Mwenyezi Mungu ni mwingi wa Rehema, basi tumuombe
awe na msamaha kwa ndugu zetu,” aliongeza.
Abdul Majham
aliyefariki dunia huko Visiwani Zanzibar na mchezaji huyo wa zamani wa klabu ya
Vikokotoni ya Zanzibar, pia aliwahi kuichezea klabu Bingwa ya kwanza ya
Tanzania, Cosmopolitan ya Dar es Salaam.
Kuhusu
Tshikungu, alifariki dunia jioni ya Oktoba 5, katika hospitali ya Peramiho
Ruvuma ambako alihamishiwa akitokea hospitali ya Ikonda iliyoko Makete mkoa wa
Njombe.
Mwenendo wa
uchezeshaji wake ulikuwa na tija kwani rekodi zinaonesha hajawahi kufungiwa au
kupewa onyo na mchezo wa mwisho kucheza ni kati ya Majimaji ya Songea na Yanga uliofanyika
Uwanja wa Majimaji mkoani Ruvuma msimu uliopita.
Tshikungu
alizikwa jana nyumbani kwake Mbeya na ameacha mke na watoto watatu mmoja kati
yao ni wa kiume.
No comments:
Post a Comment