SIMBA Queens
imeanza vema mashindano ya ligi ndogo ya wanawake baada ya kuifunga Kisarawe
Queens mabao 8-0 katika mchezo uliochezwa katika Uwanja wa Karume, Dar es
Salaam.
Katika
mchezo huo ambao ulichelewa kuanza kutokana na Kisarawe kuchelewa kufika
uwanjani huku wakiwa pungufu, Simba ilikwenda mapumziko ikiwa mbele kwa mabao
5-0.
Kipindi cha
pili Simba ambao wanaonekana kujiandaa vema waliongeza mabao matatu yalifanya
waondoke na karamu ya mabao katika mchezo huo wa ufunguzi
Akizungumza
Katibu wa Chama cha Soka la Wanawake (TWFA) Somoe Ng’itu alisema awali ligi
hiyo ilikuwa ishirikishe timu 14 ambazo zimegawanywa katika makundi mawili.
“Timu 14
zilithibitisha kushuriki lakini hadi leo ligi inaanza timu nane pekee
ndio ambazo zimefika katika kituo cha Dodoma nne na Dar es Salaam nne,” alisema
Somoe.
Katika kituo
cha Dar es Salaam timu zilizofika ni Simba Queens, Kisarawe Queens, Moro
Sisters na Tanzanite 2014 na ambazo hazijafika ni Mbinga Queens, Kilimanjaro SC na
Kwakaeza Women.
Kituo cha
Dodoma timu zilizofika ni Allans, Alliance Queens, Songwe na Mapinduzi Queens
wakati ambazo hazijafika ni Kasulu SA, Mbesco na Unyanyembe Queens.
No comments:
Post a Comment