Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, October 21, 2017

SIMBA YAIFUNGA NJOMBE MJI 4-0, YABANANA NA MTIBWA SUGAR




MZAMIRU Yassin na Emmanuel Okwi leo waliinyoosha Njombe Mji baada ya kuchangia ushindi wa mabao 4-0 kwa Simba katika mechi ya Ligi Kuu iliyochezwa Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.
Katika mechi hiyo, Yassin alifunga mabao mawili na Okwi akifunga moja huku akitengeneza mengine mawili na  Laudit Mavugo akifunga bao la nne kwa Simba.
Ni kama Okwi anawanyoosha mashabiki wanaomkebehi kwamba amezeeka na kumuita Mhenga, kwani mpaka sasa amefunga mabao nane huku timu yake ikiwa na mechi saba.
Simba imepata ushindi huo ikiwa zimesalia wiki moja kabla ya mechi dhidi ya wapinzani wake Yanga kwenye uwanja wa Uhuru mwishoni mwa wiki ijayo.
Matokeo hayo yanaifanya Simba inayohaha kusaka ubingwa kwa takribani mwaka wa tano sasa, kujikita kileleni mwa msimamo ikiwa na pointi 15 baada ya kucheza mechi saba.
Okwi alifunga bao la kuongoza kwa Simba katika dakika ya 27 baada ya kuunganisha mpira wa krosi ya Erasto Nyoni kabla ya kuujaza mpira wavuni akiwa amefikisha bao la nne msimu huu.
Simba iliyoonekana kuwa bora zaidi kwani ilifika langoni mwa Njombe Mji mara kwa mara huku wachezaji wake akiwemo Shija Kichuya wakikosa mabao kadhaa na kwenda mapumziko wakiwa mbele kwa bao hilo.
Njombe walianza kipindi cha pili wakiwa dhaifu zaidi ya kipindi cha kwanza na hapo safu ya ushambuliaji ya Simba haikufanya kosa na ndipo Mzamiru Yassin alipoandika bao la pili katika dakika ya 51 na dakika mbili baadae aliongeza la tatu. Mabao yote hayo akiunganisha pasi za ‘Mhenga’ Okwi.
Dakika ya 59, Laudit Mavugo alifunga bao la nne akiunganisha pasi ya Kichuya.
Baada ya mechi ya leo, Simba kesho itafanya safari ya Zanzibar kwa maandalizi ya mechi dhidi ya Yanga Jumamosi.
Naye Alexander Sanga kutoka Mwanza anaripoti kuwa Mbao imetoka suluhu na Azam kwenye uwanja wa CCM Kirumba.
Mechi nyingine zilizochezwa jana, Lipuli ikiwa nyumbani imeichapa Majimaji bao 1-0 Mbeya City imeifunga Ruvu Shooting mabao 2-0 kwenye uwanja wa Sokoine Mbeya, Ndanda ikitoka suluhu na Singida United na Mtibwa Sugar ikishinda bao 1-0 dhidi ya Prisons.
Mtibwa imeendelea kushika nafasi ya pili kwenye msimamo ikiwa pointi sawa na Simba, ikizidiwa mabao.

No comments:

Post a Comment