Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, October 21, 2017

DK MWAKYEMBE AIANGUKIA MALTCHOICE


WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe ameiomba kampuni ya Maltchoice Tanzania kumshika mkono katika maandalizi ya pambano la Bondia Ibrahim Class anayetarajiwa kupanda ulingoni, Novemba 28 kwenye ukumbi wa Mlimani City Dar es Salaam kutetea ubingwa wa dunia wa Global Boxig Council (GBC) kwa kupigana na bondia Hero Tito raia wa Indonesia.
Dk. Mwakyembe aliyasema hayo jana katika sherehe ya Maltchoice ya kutimiza miaka 20 ya kutoa huduma ambayo ilifanyika Dar es Salaam.
“Katika kazi zenu nimeona jinsi ambavyo mnasaidia kuendeleza michezo ikiwepo wasanii wa filamu na riadha lakini naomba mnishike mkono katika pambano la Class linatarajiwa kuchezwa hapa nchini baada ya mimi kusema litapigwa hapa nyumbani,”
“Class ni bondia kijana ana anafanya vizuri na sasa anatetea taji hilo ambalo alimpiga bondia Jose Forero raia wa Panama Julai Mosi nchini Ujerumani uzani wa kati,” aliongeza Dk. Mwakyembe.
Nje ya mkanda wa GBO pia Class anashikilia mikanda miwili ya ubingwa wa Afrika ya WBFP ambao alimpiga bondia Mwansa Kabinga wa Zambia nchini kwao na UBO alimpiga Cosmas Cheka
Class ambaye alianza Ndondi Julai 2010 ameshapigana mapambano 24 na kushinda 20 huku 10 yakiwa kwa KO na amepigwa mapambano manne moja kwa KO.

Mpinzani wake Tito alianza kupigana Februari 2004 ameshinda mapambano 23 kati yake nane ni kwa KO amepigwa 12 na kwa KO 4 na ametoka sare mara mbili.

No comments:

Post a Comment