MABINGWA wa
soka Tanzania Bara, Yanga jana walipambana na hali yao baada ya kutoka nyuma na
kulazimisha sare ya 1-1 na Majimaji katika mchezo uliofanyika mjini Songea.
Yanga
wamelalamikia Uwanja wa Majimaji kuwa ndiyo umesabaisha timu yao kutocheza vizuri
na kusababisha kuambulia sare hiyo katika mchezo huo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Kocha
msaidizi wa Yanga, Shadrack Nsajigwa alilalamikia uwanja huo na kusema kuwa
umechangia kutopata ushindi, lakini aliipongeza Majimaji kwa sare hiyo.
Kocha wa
Majimaji, Peter Mhina amewapongeza wachezaji wake na kusema kuwa walicheza
vizuri huku akisema bao la Yanga lilipatikana baada ya mabeki wake kufanya
makosa ya uzuiaji.
Mzimbabwe
Donald Ngoma ndiye aliyeiokoa Yanga isiondoke na kichapo baada ya kufunga bao
la kusawazisha katika katika dakika ya 79 kwa kichwa akimalizia krosi ya
Mzambia, Obrey Chirwa.
Majimaji
ndiyo ilikuwa ya kwanza kupata bao lililofungwa na Peter Mapunda katika dakika
ya 54 akimalizia pasi ya mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Jerry Tegete na kumfunga
kipa Mcameroon, Youthe Rostand.
Kipindi cha
kwanza wenyeji Majimaji walitawala mchezo na kufika mara nyingi kwenye eneo la
hatari la Yanga, lakini hawakuweza kufunga.
Mchezo huo
ulisimama kwa muda katika dakika ya 39 baada ya Emmanuel Martin wa Yanga
kuzimia uwanjani baada ya kugongana na mchezaji wa Majimaji Mpoki Mwakinyuke.
Kwa sare
hiyo Yanga imefikisha jumla ya pointi tano baada ya kucheza mechi tatu, baada
ya kutoka sare mara mbili na kushinda mchezo mmoja huku Majimaji wakifikisha
pointi mbili baada ya kufungwa mechi moja na sare mbili.
Kikosi cha
Majimaji kilikuwa; Andrew Ntala, Juma Salamba, Mpoki Mwakinyuke, Kennedy
Kipepe, Tumba Sued, Hassan Hamisi, Suleiman Kassim, Yakubu Kibiga/Abdulhalim
Humud, Danny Mrwanda/Jerry Tegete, Marcel Kaheza na Peter Mapunda.
Yanga;
Youthe Rostand, Juma Abdul/Hassan Kessy, Gardiel Michael, Andrew Vincent, Kevin
Yondan, Papy Kabamba Tshishimbi, Obrey Chirwa, Raphael Daudi, Donald Ngoma,
Ibrahim Hajib na Geoffrey Mwashiuya/Eammnuel Martin/Said Juma.
No comments:
Post a Comment