WEKUNDU wa
Msimbazi Simba wanashuka dimbani kesho kuwakabili Mwadui FC katika mchezo wa Ligi
Kuu Tanzania Bara kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Mchezo huo
una umuhimu kwa kila timu kushinda pointi tatu ili kujiweka kwenye nafasi nzuri
zaidi.
Simba
imeonekana kuwa mbabe wa Mwadui hasa msimu uliopita baada ya kushinda michezo
miwili, wa kwanza 2-1 kwenye uwanja wa Taifa na mwingine ulichezwa Kambarage
Shinyanga na kushinda 3-0.
Timu hiyo
ina pointi nne katika michezo miwili iliyocheza hivi karibuni ikishinda 7-0
dhidi ya Ruvu Shooting na kupata sare ya bila kufungana 0-0 dhidi ya Azam FC.
Mwadui
ilishinda mchezo mmoja mabao 2-1 dhidi ya Singida United na kufungwa na Mtibwa
Sugar 1-0 hivyo, ina pointi tatu.
Simba huenda
ikamkosa mchezaji wake muhimu Haruna Niyonzima anayesumbuliwa na majeraha.
Lakini ina furaha juu ya uwepo wa mshambuliaji wake hatari Emmanuel Okwi ambaye
hakucheza mchezo uliopita kutokana na majukumu ya timu ya taifa.
Mbali na
Okwi kuna Nicholaus Gyan ambaye anatabiriwa iwapo atacheza sambamba na Okwi
basi wapinzani watapata wakati mgumu kuwadhibiti.
Simba
inajivunia uwepo wa kipa wake mwenye kiwango kizuri Aishi Manula. Pia, mabeki
iliyonayo Erasto Nyoni, Salim Mbonde, Method Mwanjali huenda wapinzani wakapata wakati mgumu
kupenya kirahisi.
Mchezo
mwingine utakaochezwa leo ni Mbeya City dhidi ya Njombe Mji utakaochezwa kwenye
uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
Njombe
imetoka kupoteza michezo miwili kwenye uwanja wake wa nyumbani ikichapwa mabao
2-0 dhidi ya Prisons na 1-0 dhidi ya Yanga.
Mbeya City
imeshinda mchezo mmoja dhidi ya Majimaji 1-0 na kufungwa mchezo mwingine dhidi
ya Ndanda FC bao 1-0. Timu zote hizo kila moja inahitaji ushindi kujiweka
kwenye nafasi nzuri.
No comments:
Post a Comment