TIMU ya
Taifa ya soka ya Taifa ya Vijana waliochini ya miaka 15 ‘Serengeti boys’ ipo
kambini kwa ajili ya kujiandaa na mashindano ya Vijana ya Afrika yanayotarajiwa
kufanyika nchini 2019.
Timu hiyo
ambayo inaandaliwa kushiriki fainali za U-17 za Afrika 2019 ambazo Tanzania
itakuwa mwenyeji kila mwezi hukaa kambini kwa siku 21 kwa ajili ya kujenga
kikosi imara ambacho kitaleta ushindani katika fainali hizo.
Akizungumza Kocha
wa timu hiyo Oscar Mirambo alisema waliingia kambini tangu juzi na itachukua
siku 21 ili kuwafundisha wachezaji mbinu mbalimbali za soka baadae wapate
kikosi imara.
“Hii timu
ndio tunaiandaa kwa ajili ya fainali za 2019 ambazo tutakuwa wenyeji na sisi
tumejiwekea kawaida ya kukutana kila mwezi kwa wiki mbili,” alisema Mirambo.
“Huu ni
mwaka wa mwisho wa kufanya scouting hivyo wachezaji waliopatikana katika
mashindano ya Umitashumta na mashindano ya U-12 yaliyofanyika Mwanza miaka
mitatu iliyopita ndio tunaendelea kuangalia vipaji ili tubaki na wachezaji
wazuri,” alisema Mirambo
Pia Mirambo
alisema wachezaji hao wapo vizuri kwani walianza kukaa pamoja zaidi ya miaka
miwili hivyo anaamini kitakuwa kikosi kizuri kama ilivyokuwa Serengeti boys
iliyopita.
Kitendo cha
Tanzania kuwa mwenyeji wa Afcon U-17 inapata nafasi ya kushiriki moja kwa moja
hata kama itapata nafasi kwenye makundi.
Hii itakuwa
ni mara ya pili kwa timu ya Vijana kushiriki Afcon U-17 baada ya mwaka huu
kushiriki fainali za Gabon na kuondolewa kwenye hatua ya makundi.
No comments:
Post a Comment