KAMATI ya
Sheria Katiba na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), imesema
kiungo wa Yanga, Pius Buswita anaruhusiwa kucheza baada ya kuilipa Simba sh
milioni 11.
Buswita
alifungiwa mwaka mmoja baada ya Simba kumshitaki mchezaji huyo kwa kamati hiyo
kwa madai ya kuingia makubaliano na klabu hiyo lakini baadae akasajiliwa na
Yanga.
Akizungumza
na wandishi wa habari leo Mwenyekiti wa kamati hiyo Wakili Elius Mwanjala
alisema kwa sababu lengo la kamati yao ni kuona mpira unachezwa wameamua
kumfungulia Buswita baada ya makubaliano ya pande tatu ambayo Simba, Yanga na
mchezaji mwenyewe.
“Yanga
wamekubali kuilipa Simba pesa zao kwani mchezaji mwenyewe amekiri kupokea pesa
kutoka Simba na baada ya kulipwa pesa zote na kamati kujiridhisha kweli
zimelipwa ndipo ataruhusiwa kucheza,” alisema Wakili Mwanjala.
Alisema
kamati yao imetumia busara katika kumaliza shauri hilo ili kumpa nafasi
mchezaji huyo na aweze kulinda kiwango chake kwani anaweza kuwa mchezaji wa
timu ya Taifa kwani mchezaji huyo angeendelea kutumikia adhabu hiyo Simba na
Yanga ndizo zingepata hasara kwani amechukua pesa pande zote mbili.
Aidha
alisema Simba ingeweza kupeleka shauri hilo katika mahakama za kiraia kudai
haki yao kwa sababu mchezaji huyo alisaini wakati wa kuchukua pesa hizo
shilingi milioni 10 pamoja na gharama ya tiketi za ndege ambayo ni shilingi
milioni moja zilizotajwa na Simba kwenye barua yao waliyoiwasilisha TFF.
Wakili
Mwanjala alisema kamati imetoa onyo kali la kimaandishi kwa mchezaji huyo pia
wameagiza timu zote kuwalipa wachezaji pesa za usajili (sign fee) mapema iwezekanavyo
na endapo mchezaji atakuwa hajalipwa anatakiwa kuwasilisha malalamiko yake ili
zikatwe kwenye malipo ya klabu.
Buswita alijiunga
na Yanga akitokea Mbao FC ya Mwanza alifungiwa na kamati hiyo baada ya
kusajiliwa na Yanga huku pia akiwa amesaini mkataba na Simba.
No comments:
Post a Comment