UONGOZI wa
Chama cha Waamuzi wa soka Taifa (FRAT) kimesimamisha mafunzo yote ya waamuzi
wapya hadi hapo kitakapotangaza tena.
Akizungumza
jana, Mwenyekiti wa FRAT, Joseph Mapunda alisema kamati ya utendaji iliyokaa
Septemba 6-7 ndio iliyoamua kusimamisha ili kuweka mitihani mipya kulingana na
mabadiliko ya sheria za soka.
“Tunataka
kufanya kujua wakufunzi wanaofundisha kuanzia ngazi ya chini kama ni watu
sahihi ili kusaidia kupata waamuzi bora,”.
“Mitihani
iliyofanywa kabla ya Septemba 7 ni sahihi na tutaipokea ikiwa imeambatanishwa
na ada zake pia mwisho wa kulipa ada kwa wanachama ni Februari 28,” alisema
Mapunda.
Pia chama
hicho kimesema kila mwanachama anatakiwa kulipa ada kwenye chama chake cha mkoa
au wilaya na endapo mtu atachelewa kulipa ada watawasiliana na TFF ili
kuwaondoa kwenye ratiba wale wanaochezesha ligi na makamishna.
Aidha
alisema kila mkoa unatakiwa kulipa ada ya ushiriki ambayo ni sh. 30,000 badala
ya sh. 20,000 na kila mkoa kuwa na darasa la kila mwisho wa wiki.
Mapunda
alisema watakuwa wanazalisha waamuzi wapya kupitia shule za sekondari na vyuo
ili kupata waamuzi bora ambao baadae watakuwa viongozi au wakufunzi.
No comments:
Post a Comment