Beki wa Yanga akiwania mpira na beki wa Mtibwa, Stahimili Mbonde (kulia) wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Tanznaia Bara uliochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam leo na kumalizika kwa suluhu. |
Mashabiki hawaamini kuwa dakika 90 zimeisha kwa suluhu |
Daktari Bavu akimwangalia Ngoma |
YANGA imeshindwa
kutumia vema uwanja wake wa nyumbani baada ya kulazimishwa suluhu na Mtibwa
Sugar katika mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru,
Dar es Salaam
Hii ni sare ya tatu
kwa Yanga tangu kuanza msimu huu baada ya kutoka suluhu na Lipuli kabla ya kutoka
sare ya bao 1-1 na Majimaji na kwa Mtibwa ni ya pili.
Matokeo hayo
yanaifanya timu hiyo ishike nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi ikiwa na
pointi tisa.
Katika mchezo huo timu
zote zilishambuliana kwa zamu, wenyeji
Yanga wakitawala kipindi cha kwanza na wageni kipindi cha pili.
Yanga ilianza kukosa
mabao kuanzia dakika ya 26 ambapo Ibrahim Ajib alipiga shuti kali
lililopanguliwa na kipa wa Mtibwa Sugar, Benedict Tinoco.
Yanga ilikosa bao
lingine katika dakika ya 52 ambapo mchezaji wake, Raphael Daudi shuti lake
lilipanguliwa na kipa wa Mtibwa, Tinoco.
Aidha Mtibwa ilikosa
bao katika dakika ya 60 ambapo shuti la Salum Kihimbwa lilipanguliwa na kipa wa
Yanga, Youthe Rostand.
Kwenye uwanja wa
Jamhuri Dodoma, wenyeji Singida United wamepunguzwa kasi baada ya kulazimishwa
sare ya bao 1-1 na Azam.
Matokeo hayo
yanaifanya Mtibwa na Azam kuendelea kulingana pointi baada ya zote kuwa na
pointi11, Mtibwa ikiongoza kwa uwiano mzuri wa mabao.
Huko Mwanza wenyeji
Mbao walilazimishwa sare ya bao 1-1 na Prisons, wenyeji wakichomoa bao hilo
dakika za mwisho.
Bao la wageni Prisons
lilifungwa na Eliuter Mpepo katika dakika ya 48 na lile la Mbao likifungwa na
Rajesh Kotecha dakika ya 84.
Aidha mechi nyingine
zilizochezwa Mwadui ililazimishwa sare
ya mabao 2-2 nyumbani dhidi ya Mbeya City, Majimaji ikitoka suluhu nyumbani
dhidi ya Kagera Sugar na Ruvu Shooting ikilazimishwa sare ya bao 1-1 na Njombe
Mji.
No comments:
Post a Comment