WANACHAMA 1,216
wa Simba wamepitisha uamuzi wa klabu yao kuingia kwenye mfumo wa hisa kwa kura
za wazi huku mmoja pekee akipinga.
Mkutano huo
ulifanyika katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere ulikuwa na ajenda tisa lakini
ajenda kuu zilikuwa tatu ambazo zilihusu mabadiliko ambayo ni kuwasilisha
mapendekezo kwa wanachama, kujadili na kupiga kura kama mfumo huo utakubaliwa
ama kukataliwa.
Katika
mkutano huo ambao umehudhuriwa na wanachama 1217, wanachama 1216 walikubali
wawekezaji kumiliki asilimia 50 na wenyewe kubaki kuwa wamiliki kwa asilimia 50
huku mmoja pekee akikataa baada ya kuhojiwa na Kaimu Rais wa Simba Salim
Abdallah ‘Try Again’,
Pia Salum
Abdallah alisema wawekezaji mmoja, wawili au watatu watatakiwa kutoa Sh bilioni
20 katika uwekezaji huo sawa na wanachama.
“Kwa sababu
wanachama wanaonekana si wenye uwezo wa kutosha kifedha watatakiwa kuchangia Sh
bilioni nne tu ambazo nia silimia 10 huku 40 ambayo ni sh. bilioni 16 zitawekwa
kando kwa kuangalia uwezo wao,” alisema Salim Abdallah.
Kabla ya
kuanza kujadiliwa agenda ya mabadiliko mwanasheria wa Simba, Evodius Mtawala
aliwaeleza wanachama hao umuhimu wa kuingia kwenye mfumo huo kulingana na ibara
ya 49 kifungu kidogo cha 3.
“Mtakachokiamua
leo itaundwa kamati kuu huru ya wataalamu ambayo itaandaa mkutano na kuwaita
kuwaeleza ni nani waliojitokeza na wanachama mtaamua ni nani atakuwa mwekezaji,”
alisema Mtawala.
Pia Mtawala
alisema kabla ya kuingia kwenye mchakato huo kamati ya utendaji itakaa na
kuhakiki uanachama ili kupata orodha halisi ya wanachama na kuingiza kwenye
leja
Naye
mdhamini mpya wa Simba, Adam Mgoyi
ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Kilosa aliwashukuru wajumbe kwa kumchagua kuwa
mmoja wa baraza la wadhamini huku akiwa na umri mdogo.
“Nawashukuru
kwa kuniamini kuwa dhamana ya kusimamia mali za klabu za Simba na nawaahidi
kutokuwa na hila wala mbinafsi kwani mmenichagua baada ya kugongwa na nyoka
kwani maana ya kuwa mdhamini ni kusimamia kulingana na sheria mali za klabu na
nitashirikiana na wenzangu katika maamuzi mtakayofikia,” alisema Mgoyi.
“Niwashukuru
viongozi kwa kuwezesha kuingia kwenye mfumo mpya kwani klabu ya Simba ina zaidi
ya miaka 80 na wamefanikiwa kupitisha mabadiliko kwa kufuata utaratibu na wale
ambao watakuwa hawajaelewa wanaruhusiwa kuuliza,” alimaliza Mgoyi.
Naye Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Hamis
Kigwangala na Makamu wa Rais wa TFF, Wambura waliwashukuru viongozi kwa
kufanikiwa kuingia kwenye mfumo na kuomba wanachama kuwa watulivu na kuahidi
kutoa ushirikiano kwaq uongozi.
Mabadiliko
ya mfumo wa uendeshaji yalikuja baada ya mfanyabiashara, Mohamed Dewji ‘Mo’
kuonyesha nia ya kutaka kuwekeza Sh 20 bilioni huku yeye akihitaji kumiliki
hisa asilimia 51 ingawa mkutano wa wanachama mmiliki wa hisa nyingi atakuwa na
asilimia 50.
Mkutano huo
ulihudhuriwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto, Dk Hamis Kigwangala, Kaimu Rais wa Simba Salim Abdallah ‘Try Agano’,
Makamu wake Idd Kajuna.
Wengine ni
wadhamini wa klabu hiyo Ramesh Patel, Adam Mgoyi na Juma Kapuya pamoja na
Makamu wa Rais wa shirikisho la soka nchini (TFF), Michael Wambura ambaye ni
mwanachama wa Simba.
No comments:
Post a Comment