MBAO FC ya
Mwanza imeingia mkataba wa udhamini wa mwaka mmoja na kampuni ya GF Trucks
& Equpments wenye thamani ya sh. milioni 140.
Akizungumza na wandishi wa habari leo Ofisa Masoko wa kampuni hiyo, Kulwa Bundala alisema katika mkataba huo Mbao itapata basi lenye thamani ya sh. milioni 70 pamoja na fedha taslimu sh. milioni 70.
Akizungumza na wandishi wa habari leo Ofisa Masoko wa kampuni hiyo, Kulwa Bundala alisema katika mkataba huo Mbao itapata basi lenye thamani ya sh. milioni 70 pamoja na fedha taslimu sh. milioni 70.
“Tumeingia
mkataba wa mwaka mmoja na Mbao kwa sababu tumeona jitihada zao katika mchezo wa
soka na tunasaini mkataba wenye thamani ya shilingi milioni 140 na ndani
ya mkataba huo tunawapatia basi lenye thamani ya shilingi milioni 70 na milioni
70 nyingine tutawakabidhi fedha taslimu,”.
Pia Bundala
aliipongeza Mbao FC kwa kuanza ligi vizuri kwani waliifunga Kagera Sugar katika
mchezo wa ufunguzi wa ligi kuu ikiwa ni msimu wake wa pili tangu ipande ligi
kuu lakini imeweza kufanya vizuri.
Naye Mwenyekiti wa klabu hiyo Solly Zephania Njashi aliishukuru kampuni
ya GF kwa kuingia nao mkataba nakusema basi litawasaidia katika safari
mbalimbali kipindi hiki cha ligi.
“Tunawashukuru
GF kwa udhamini wao wa fedha pamoja na basi kwani itasaidia kwenye klabu yetu katika
safari za mikoani za ligi kuu,” alisema Solly.
Huo ni udhamini
baada ya mwaka jana kupata udhamini wa Hawaii Products Supplies, watengenezaji
wa maziwa ya Cowbell wenye thamani ya sh. milioni 50 kwa msimu.
Katika msimu
uliopita Mbao ni washindi wa pili wa Azam Sports Federation Cup.
No comments:
Post a Comment