MSHAMBULIAJI
wa Azam FC, Ramadhan Singano ‘Messi’ ameongeza mkataba wa miaka miwili
kuendelea kuitumikia klabu hiyo baada ya kukwama kusaini mkataba na El Jadidi
ya Moroco alikofauli majaribio yake.
Singano
alirejea jijini Dar es Salaam juzi baada ya wakala wake kutokuwa mwadilifu
katika makubaliano ya kimkataba kwani inadaiwa aliongeza dau mara mbili ya ile
waliyokubaliana awali.
Akizungumza
na gazeti hili, Ofisa habari wa timu hiyo Jaffa Idd alisema uongozi umeamua
kumpa mkataba mpya kwa sababu wakati anaondoka aliaga na akapata baraka zote na
akaambiwa endapo atakwama anaruhusiwa kurudi.
“Singano tulimwambia akikwama arudi nyumbani
tutampa mkataba, kijana wetu alikwenda kutafuta maisha lakini mambo yamekuwa
tofauti na matarajio yake, alichanganyikiwa ila anapaswa kutulia acheze mpira,”
alisema Jaffar Idd
Naye Singano
amekiri kuongeza mkataba na kuishukuru Amaz kwa kuonesha utu kwa hata alipokuwa
Morocco walikuwa wanamfuatilia kwa karibu.
“Ni kweli
nimepewa mkataba mpya, Azam wamenifanyia utu kwani hata nilipokuwa Morocco
walikuwa wakiwasiliana na mimi kujua maendeleo yangu, hata nilipokuwa naondoka
waliniahidi hilo kwamba nikishindwa nirudi nyumbani,” alisema Messi
Singano
atakuwemo kwenye kikosi cha Azam ambacho kitaondoka kesho kwenda Kampala,
Uganda kuweka kambi maalumu ya maandalizi ya msimu mpya wa ligi utakaonza
Agosti 26.
No comments:
Post a Comment