WAKATI Kamati ya Uchaguzi ikimrejesha Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ kwenye kinyanganyiro cha Uchaguzi Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania, wagombea wengine wanne wameenguliwa na kamati hiyo.
Akizungumza
na wandishi wa habari leo, Mwenyekiti wa kamati hiyo, Wakili Revocatus Kuuli
alisema kamati yake imewaondoa Shaffih Dauda, Elias Mwanjala, Benista Lugola na
Ephraim Majige ambao walikuwa wanagombea ujumbe wa kamati ya utendaji.
“Tumejidhisha
kuwa Julio ni kweli alisoma Kinondoni Muslim baada kupata vithibitisho kutoka
baraza la mitihani lakini pia tumewaengua wagombea wanne ambao walikamatwa na
TAKUKURU hivu karibuni kule Mwanza,” alisema Kuuli.
Pia Wakili Kuuli
kamati yao imewaondoa wagombea hao lakini pia wana haki ya kukata rufaa kabla
ya kamati yao kukaa Jumanne ya wiki ijayo kutoa orodha ya mwisho ya wagombea
wote ili kuanza kampeni.
Jumla ya wagombea 74 walichukua fomu huku 58
wakiwania nafasi za ujumbe wa kamati ya utendaji katika Kanda mbalimbali hivyo
kuondolewa wanne wanabaki 54 huku wagombea 10 wakiomba nafasi urais na makamu
rais sita.
Uchaguzi Mkuu unatarajiwa kufanyika Agosti 12
mkoani Dodoma.
No comments:
Post a Comment