MGOMBEA wa
Urais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Shija Richard Shija amesema atajenga
shule ya kukuza vipaji na kuviendeleza mkoani Dodoma na kila mkoa ataajiriwa
mratibu wa soka.
Shija
aliyasema hayo jana wakati akizindua kampeni zake na kusema ili upate matokeo
mazuri katika soka lazima wachezaji waanze kuandaliwa wakiwa na miaka sita
hivyo ataweka mfumo rasmi wa kukuza na kuendeleza vipaji.
“ Kampeni
zangu zitajikita katika kutangaza mambo ya kisera ya TFF badala ya masuala ya
kiutendaji kwani mafanikio katika soka
sio jambo la kufumba na kufumbua,” alisema Shija.
Shija
alisema Tanzania ina changamoto kubwa katika mfumo rasmi wa kutambua na
kuendeleza wachezaji hivyo amekuja na mpango wa muda mrefu na muda mfupi.
Pia Shija
alisema mratibu wa soka atakayeajiriwa kila mkoa atakuwa anaripoti kwa
mkurugenzi wa ufundi wa TFF na atakuwa
na jukumu la kutoa mapendekezo ya wachezaji wanaostahili kupelekwa katika shule
ya vipaji.
Aidha Shija
alisema atasimamia na kutekeleza Azimio la Bagamoyo lililoanzishwa na uongozi
uliopita kwa sababu linagusa mambo muhimu ya kuendeleza soka.
Alisema
ataimarisha misingi imara mikoani kwa sababu mikoani ndiko unakochezwa soka kwa
hatua za awali ili kuongeza ari ya kushiriki na kuwekeza katika michezo.
Alisema
atajenga miundombinu na mazingira rafiki ya kucheza mpira na kuwashawishi
wazazi kuwekeza na kuwaruhusu watoto wao wenye vipaji waingie kwenye michezo.
Shija
alisema atahakikisha timu zinaajiri watendaji wenye weledi wa kutosha na
kuahidi kushirikiana na vyama wanachama wa TFF na kuimarisha soka.
No comments:
Post a Comment